Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:06

Mkwaju wa penalti waupatia Equatorial Guinea ushindi wa kihistoria


Wachezaji wa Equatorial Guinea walindwa na polisi baada ya ushindi dhidi ya Tunisia
Wachezaji wa Equatorial Guinea walindwa na polisi baada ya ushindi dhidi ya Tunisia

Fujo na ngumu za gubika matokeo ya kihistoria ya Equatorial Guinea, kuilaza Tunisia mabao mawili kwa moja na kusonga mbele kwa mara ya kwanza katika nusu finali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.

Mkwaju wa penalti ulokuwa na utata ulotolewa dakika 90.30 ikiwa ni wakati wa dakika za majeraha na kutumbukizwa wavuni na Javier Balboa, ulisababisha mcehzo wa robo finali mjini Bata kuingia katika muda wa ziada.

Mnamo dakika ya 12 ya muda wa ziada, Balboa kwa mara nyingine alipachika mkwaju mzuri sana kutokana na freekick na kuipatia ushindi timu yake ya Nzalanga, yani radi, ushindi ambao haujapata kushuhudiwa na nchi hii.

Tunisia iliyokuwa inaongoza wakati wote kutokana na bao zuri la Ahmed Akaichi, katika dakika ya 70, ilipigwa na buta na wachezaji kuanza kucheza mchezo ambao uliharibu kabisa hadhi ya michuano ya maka huu 2015 , kwa kuwaangusha na hata kuwapiga ngumu wachezaji wa Equatiorial Guniea muda wote ulobaki wa ziada na hata klumlazimisha referee kupiga kipengele cha mwisho dakika mbili kabla.

Hili lilikuwa pigo baya zaidi kwa Tunisia katika historia yake ya kandanda ya miaka 58, kushindwa baada ya kuongoza muda wote wa mchezo na kushindwa na timu iliyonafasi 96 chini yake katika orodha ya timu boira ya kandana kulingana na FIFA.

Polisi wanawatenganisha maafisa wa CAF kutoka wachezaji wa Tunisia wenye hasira CAN 2015
Polisi wanawatenganisha maafisa wa CAF kutoka wachezaji wa Tunisia wenye hasira CAN 2015

Vurugu lilizuka uwanjani na kulazimisha polisi wa usalama na wale wa kukabiliana na ghasia kuingia uwanjani kutenganisha wachezaji na kumlinda referee aliyepigwa ngumi pia na mchezaji wa Tunisia.

Wachambuzi na mashabiki wameshtushwa na matokeo hayo ambayo yatakumbukwa kama tukio baya zaidi katika michuano 30 ya finali za AFCON. Maafisa wa CAF wanatazamiwa kutoa taariofa karibuni juu ya matokeo hayo yote.

XS
SM
MD
LG