Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:10

Timu za kundi D kuamua hatima yao Jumatano


Bakary Sako ewa Mali , (kulia akizuiliwa na Benjamin Moukandjo, kushoto wa Cameroon wakati wa Kombe la Mataifa Afrika kundi D mjini Malabo
Bakary Sako ewa Mali , (kulia akizuiliwa na Benjamin Moukandjo, kushoto wa Cameroon wakati wa Kombe la Mataifa Afrika kundi D mjini Malabo

Awamu ya tatu na ya mwisho ya makundi katika Kombe la Matifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea inafikia kikomo siku ya Jumatano wakati timu nne za kundi D zitakapokutana uwanjani

Timu zote nne zimekwenda sare moja kwa moja, na hiovyo kufanya hali kuwa ngumu zaidi kuliko ilivyokua makundi mengione matatu. Na wakati Cameroon watakapokutana na Ivory Coast, mjini Malabo na Mali kupambana na Guinea mjini Mongomo na kutoka sare basi itabidi kupitia njia ya bahati na sibu.

Hali hiyo ikitokea haitakuwa ni mara ya kwanza kufanyika hivyo, kwani itakumbukwa kwamba mwaka 1988 wakati wa Kombe la Mtaifa ya Afrika Algeria ilkiweza kuingia katika robo fainali badala ya Ivory Coast ambazo zilikwenda sare katika michuano yao yote ya awali.

XS
SM
MD
LG