Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:18

Ushindi wa Ghana waashiria mashindano makali kundi C


Ghana na Algeria zinashuka uwanjani Mongomo Ijuma 23, 2015
Ghana na Algeria zinashuka uwanjani Mongomo Ijuma 23, 2015

Ushindi wa Ghana dhidi ya Algeria huko Mongomo siku ya Ijuma umeleta mabadiliko makubwa na hali ya kufa na kupona kwa timu za kundi C ili kugombania nafasi ya kuingia robo finali. Hivi sasa Aligeria, Ghana na Senegal zimeshapata ushindi wa point tatu ingawa Algeria ina kuwa na pointi 3 baada ya kushindwa.

Katika mchuano wa kuvutia Ghana ili weza katika dakika mbili za majeraha kujipatia goli pekee kutoka mchezaji wake Asamoah Gyan mwisho kupitia na hivyo kuiweka Algeria inayochukuliwa kama timu bora ya Afrika kwa wakati huu na FIFA ukingoni.

Senegal mbayo inawachezaji wengi kutoka Ulaya haikuweza kupenya ukuta waulinzi wa vijana wa Bafana Bafana kutoka Afrika kusini, na hivyo kulazimika kwenda sare moja kwa moja.

Matokeo hayo yanaifanyan kinyan’ganyiro kuwa ngumu hivi sasa, kwani yeyote anayetaka kusonga mbele lazima apate ushindi wakati wa mchezo wao wa miwsho.

Hivi sasa Senegal inaongoza ikiwa na pointi nne ikifuatwa na Ghana point 4, Algeria pointi tatu na na Afrika ya Kusini ina moja na watalazimika kiufiunga virago na kurudi nyumbani lakini wataweza kuharibia timu ya Ghana ikijipatia ushindi siku ya Jumanne.

Hali si tofauti katika makundi mengi kutokana na kwamba timu nyingi zimekwenda sare katika michunao yao ya awamu ya makundi, na kusababisha michuano ya mwishoni mwa wiki na mapema wiki ijayo kuwa ya kuvutia zaidi.

XS
SM
MD
LG