Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:45

Polisi wa DRC wawauwa vijana wengi kupambana na uhalifu: Human Rights Watch


Mkurugenzi wa kitengo cha Afrika katika Human Rights Watch, Baniel Bekele
Mkurugenzi wa kitengo cha Afrika katika Human Rights Watch, Baniel Bekele

Kundi la haki za binadamu linasema polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC wamewaua darzeni ya vijana wakati wa kampeni dhidi ya uhalifu iliyoanza mwaka mmoja uliopita.

Kundi la Human Rights Watch lenye makao makuu yake Marekani ilitoa ripoti Jumanne ambayo ilisema kwamba “Operesheni Likofi” ilisababisha vifo vya watu wasiopungua 51 na kupotea kwa watu wasiopungua 33 wengine walioshukiwa kuwa katika genge la uhalifu.

Kampeni hiyo ilidumu kutoka Novemba mwaka 2013 hadi Februari mwaka 2014.

Ripoti ya Jumanne ilimnukuu mkurugenzi wa Human Rights Watch kwa upande wa Afrika, Daniel Bekele, akiwataka maafisa wa Congo kuchunguza mauaji hayo, kuanzia kamanda wa operesheni hiyo na kuwafikisha watu waliohusika kwenye vyombo vya sheria.

Imeendelea kusema, polisi waliwakamata watuhumiwa wa kundi linalojulikana kama “kaluna” kutoka majumbani mwao usiku na kiwapiga risasi nje ya nyumba zao, ama kwenye masoko walipokuwa wamelala ama kufanya kazi.

Vilevile ripoti imesema watuhumiwa wengine walichukuliwa bila hati za kukamatwa na kupotea. Ripoti imeongeza mwanzoni polisi waliwaonya watu kwa kuwapiga hadharani ama kuacha miili ili watu waone.

XS
SM
MD
LG