Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:36

Africa yapoteza msomi Profesa Ali Mazrui


Professor Ali Mazrui akizungumza katika chuo kikuu cha Fayetteville, Carolina ya Kaskazini
Professor Ali Mazrui akizungumza katika chuo kikuu cha Fayetteville, Carolina ya Kaskazini

Msomi na mtaalamu wa masuala ya kisiasa na dini ya Kislamu, Profesa Ali Mazrui amefariki mjini Binghamton, jimbo la New York, Marekani akiwa na umri wa miaka 81, baada ya kuugua kwa muda fulani.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho na Seneta Hassan Omar walitangaza kifo cha msomi huyo maarufu na kueleza kwamba matayarisho ya maziko yake yananaza kufanyika huko Mombasa.

Joho alisema jimbo la Pwani na Kenya kwa ujumla wamempoteza mtu muhimu, msomi, profesa wa taaluma za Kislamu na masuala ya Afrika. Anasema Profesa Mazuri alisihi kuzikwa Mombasa katika mtaa mashuhuri wa jumba la makumbusho la Fort Jesus.

Alikua mkurugenzi wa taasisi ya Taaluma ya Utamaduni wa Kimataifa, katika chuo kikuu cha Binghamton. Yeye ni msomi anayfahamika kote duniani na amesomesha katika mabara yote matano ya dunia na kuandika karibu vitabu 30.

Profesa Mazurui aliyezaliwa Februari 24 1933, alikua mchambuzi mkuu wa vyombo vya habari pamoja na Sauti ya Amerika.

Amewaacha mjane na watoto sita.

XS
SM
MD
LG