Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:20

Mkuu wa idara ya usalama maalum Marekani ajiuzulu


Mkuu wa idara ya usalama maalum Marekani Julia Pierson
Mkuu wa idara ya usalama maalum Marekani Julia Pierson

Mkuu wa idara ya usalama maalum Marekani amejiuzulu wadhifa wake kufuatia ukiukaji mkubwa wa kanuni za kiusalama ikiwemo tukio la septemba 19 ambapo mtu mmoja aliyekuwa na silaha aliweza kuingia ndani katika makazi ya rais.

Mkurugenzi wa idara ya usalama wa ndani Julia Pierson aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa waziri wa usalama wa ndani Jumatano siku moja baada ya kuhojiwa vikali na wabunge kuhusu mtu aliyekuwa na kisu aliyeweza kuruka ukuta na kuingia ikulu mwezi Septemba.

Wakati wa kutoa ushahidi wake mbele ya kamati ya bunge siku ya Jumanne, Pierson alikubali uzembe ndani ya shirika lake.

Alisema ni wazi kwamba mpango wao wa usalama haukutekelezwa inavyotakiwa. Hillo halikubaliki na anawajibika kikamilifu na kuhakikisha kwamba kosa hilo halitokei tena.

Masaa kadhaa baada ya mahojiano hayo vyombo vya habari viliripoti ukiukwaji mwingine wa hatua za kiusalama, ambapo wakala wa ulinzi aliyekuwa na silaha mwenye rekodi za uhalifu alikuwa sentimita chache kutoka kwa rais Obama katika eleveta, wakati rais alipotembelea kituo cha kudhibiti magonjwa huko Atlanta , Georgia septemba 16.

Msemaji wa white house Josh Earnest aliwaambia waandishi wa habari rais Barack Obama aligundua juu ya tukio hilo muda mfupi kabla ya kutangazwa.

Ernest alisema rais aliendelea kuliamini shirika la usalama wa ndani na kukubali kujiuzulu kwa Pierson kwa sababu alikubaliana na tathmini yake kwamba ilikuwa ni kwa manufaa ya shirika hilo.

XS
SM
MD
LG