Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:47

ANC yaongoza kura za awali Afrika Kusini .


Rais wa Afrika Kusini na kiongozi wa chama cha ANC, Jacob Zuma, akipiga kura huko eneo la Ntolwane, katika jimbo la KwaZulu Natal, Afrika Kusini, akipiga kura yake Jumatano , Mei 7, 2014.
Rais wa Afrika Kusini na kiongozi wa chama cha ANC, Jacob Zuma, akipiga kura huko eneo la Ntolwane, katika jimbo la KwaZulu Natal, Afrika Kusini, akipiga kura yake Jumatano , Mei 7, 2014.
Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kinaongoza katika idadi ya kura za awali katika uchaguzi wa kwanza wa nchi nzima ukijumuisha wapiga kura waliozaliwa baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Matokeo ya awali yaliyotolewa na tume ya uchaguzi nchini humo alhamisi yanaonyesha ANC ikiwa na asilimia 62 ya kura huku ikiwa kiasi ya nusu ya kura zimehesabiwa.

Wapinzani wao wa karibu Democratic Alliance walikuwa na asilimia 24. Na hakuna chama kingine chochote kilichopata zaidi ya asilimia 5 katika kura zilizohesabiwa mpaka sasa.

Tume ya uchaguzi ilisema asilimia 73 ya wapiga kura halali walishiriki katika maeneo ya upigaji kura wa jumatano.

Wachambuzi wanatarajia ANC kupata zaidi ya asilimia 60 ya kura .Hiyo itasafisha njia kwa bunge kumchagua rais Jacob Zuma kwa muhula mwingine wa miaka mitano.
XS
SM
MD
LG