Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:11

Juhudi za kuwatafuta watu 290 baada ya meli kuzama zaendelea Korea Kusini


 Helikopta inaonekana ikienda kusaidia abiria 476 waliokuwamo kwenye meli ya Korea kusini iliyozama.
Helikopta inaonekana ikienda kusaidia abiria 476 waliokuwamo kwenye meli ya Korea kusini iliyozama.
Maafisa wa Korea kusini wanasema watu wanne wamefariki na wengine 290 hawajulikani walipo baada ya meli kuzama kwenye pwani ya kusini ya nchi hiyo Jumatano.

Meli hiyo ilikuwa na abiria zaidi ya 459 wengi wao walikuwa wanafunzi waliokuwa wakielekea kwenye kisiwa cha mapumziko cha Jeju, ilizama katika wakati ambapo hali baharini ilionekana kuwa ya utulivu.

Wengi wanahofiwa kuwa wamenasa ndani ya meli hiyo iliyozama au kukwama katika maeneo ya karibu ya majini ambayo ni ya kiasi cha joto la Celsius 12.

Dazeni ya helikopta na meli ikiwa ni pamoja na za jeshi la Marekani ikiwa ni pamoja na meli ya kijeshi ya Marekani Amphibia zinashiriki katika operesheni kubwa ya utafutaji na uokozi.
Kikosi cha wanajeshi wanamaji wa Korea Kusini “Navy Seal” wanatafuta meli hiyo iliyozama lakini maafisa wanaonya kuwa wale waliokwama ndani huenda wamepoteza maisha.

Walionusurika walipelekwa kwenye kisiwa cha karibu cha Jindo.Kim Tae-young mwanafunzi anasema alichukua hatua haraka wakati meli inaanza kuzama.

Abiria wengi wanasema mwanzo waliambiwa wabaki kwenye viti vyao wasijaribu kukimbia.Yoo Ho-shil anasema alipoona meli inaanza kuzama ilibidi achukue hatua haraka.
XS
SM
MD
LG