Jumapili, Mei 24, 2015 Local time: 20:04

Habari / Afrika

DRC: Kundi la waasi M23 lamshika mateka Mtanzania.

Wanajeshi wa serikali ya congo katika eneo la mapigano na kundi la M23.Wanajeshi wa serikali ya congo katika eneo la mapigano na kundi la M23.
x
Wanajeshi wa serikali ya congo katika eneo la mapigano na kundi la M23.
Wanajeshi wa serikali ya congo katika eneo la mapigano na kundi la M23.

Kundi la waasi la M23 nchini Drc limedai kumkamata mtu mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Christopher George Yohana katika hati yake ya kusafiria akipigana sambasamba na  jeshi la serikali FARDC kupambana na kundi la M23 katika maeneo ya kibati nchini DRC.

Msemaji wa kundi la M23 Vernnei Kazarama ameiambia sauti ya amerika kwa njia ya simu kwamba kijana huyo anayesadikiwa kuandikishwa na serikali ya congo kama mwanajeshi wa Tanzania amejieleza na kukubali kwamba anatokeo nchi jirani ya Tanzania.

Mapigano yenye ghasia kubwa yalitawala Jumatatu ikiwa ni mwendelezo wa ghasia za mapigano mapya yaliyozuka julai 10 huko kivu kaskazini na kulazimisha maelfu ya watu kukosa makazi na kutorokea nchi jirani ya Uganda.

Kazarama amesema kama serikali ya Tanzania itaomba kuachiliwa mwanajeshi huyo kutoka tanzania kwa njia ya kipiplomasia au kupitia shirika la msaba mwekundi M23 iko radhi kumwachilia huyu mateka huyo.

Hata hivyo ameishutumu nchi ya Tanzania akisema kuwa imekuwa ikiruhusu wapiganaji kutoka Tanzania kusaidiana na vikosi vya serikali ya Congo badala ya wale wa ulinzi wa amani wa umoja wa mataifa.

Jumatatu kundi la M23 ilisambaza hati ya kusafiria yenye majina kamili na utaifa wa mateka huyo ikidai kwamba inataka kutuma ujumbe kwa dunia nzima kwamba Tanzania inaisadia Drc katika uvunjifu wa amani.

Sauti ya ameriba bado inaendelea kuitafuta serikali ya tanzania ili kutoa ufafanuzi zaidi juu ya maelezo yaliyotolewa na kundi la waasi la M23.
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.