Jumatano, Aprili 23, 2014 Local time: 11:54

Habari / Afrika

Rasimu ya katiba mpya ya Tanzania yatangazwa

Waandamanaji wanataka mageuzi ya katiba yafanyike Tanzania kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Waandamanaji wanataka mageuzi ya katiba yafanyike Tanzania kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
ukubwa wa habari - +
Dinah Chahali
— Tanzania imeingia katika historia mpya Jumatatu baada ya kusomwa kwa rasimu ya awali ya katiba ya nchi hiyo iliyotolewa na tume ya mabadiliko ya katiba ikiwa imependekeza masuala kadhaa yatakayobadili muundo wa serikali ya nchi hiyo.

Miongoni mwa mambo makuu yaliyopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba katika rasimu hiyo ya awali ya katiba ni pamoja na kuwa na muungano wa serikali tatu, yaani ya Shirikisho, ya Tanznaia bara na Zanzibar huku mambo ya muungano yakipunguzwa kutoka 22 ya sasa hadi kubaki saba.

Aidha tume ya mabadiliko ya katiba imependekeza kuwa spika wa bunge na naibu wake asitoke kwenye wabunge au chama chochote cha siasa na pia kuweka ukomo wa mtu kuwa mbunge ambapo sasa itakuwa mwisho vipindi vitatu. Tume ya mabadiliko ya katiba pia imependekezwa kufutwa kwa wabunge wa viti maalum na wabunge wa muungano kuwa 75, 20 kutoka Zanzibar na 50 Tanzania bara huku watano watateuliwa na rais kutoka kundi la watu wenye ulemavu.

Ripoti ya Dinah Chahali
Ripoti ya Dinah Chahali - 2:53i
|| 0:00:00
...
 
🔇
X

Kwa upande wa tume ya uchaguzi. Tume ya mabadiliko ya katiba imependekeza tume kuitwa Tume Huru ya Uchaguzi ambapo sifa za kuwa mjumbe wa tume hiyo huru ya uchaguzi zitaainishwa kwenye katiba na pia kuwa na kamati maalum ya uteuzi wa wajumbe. Majukumu ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa yataunganishwa kwenye  tume huru ya uchaguzi

Tume ya mabadiliko ya katiba pia imependekeza kuruhusiwa mgombea binafsi kutoka ngazi ya chini hadi urais, hata hivyo imeacha umri wa miaka 40 kuwa ndio wa kuanzia mtu kuruhusiwa kugombea urais..Aidha wamependekeza mawaziri wa muungano wasizidi 15 na uteuzi wao utathibitishwa na bunge..

Jambo lingine kubwa walilopendekeza tume ya mabadiliko ya katiba kuwepo kwenye rasimu hiyo ya awali ya katiba ni pamoja na kuwa na haki ya kuhoji matokeo ya urais katika mahakama ya juu zaidi waliyopendekeza iwepo kwenye katiba, lakini kwa yule tu aliyegombea urais  na kwamba mshindi wa urais atatangazwa iwapo atapata zaidi ya asilimi 50 ya kura zote.

Asha Rose Migiro naibu katibu mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa alizungumzia suala la mgombe binafsi na kutaka umakini utumike katika kujadili na hatimaye kufikia muafaka kutokana na unyeti wa suala lenyewe..

Peter Kuga Mziray aliwakalisha vyama vya siasa..katika uzinduzi huo wa rasimu ya awali ya katiba..na kupongeza tume ya mabadiliko ya katiba kuweka mambo kadhaa ambayo wapinzani walikuwa wakiyapigania ikwemo muunda wa muungano wa serikali tatu na suala la Rais kupata zaidi ya asilimia 50

Rasimu hii ya awali ya katiba ndiyo itakayojadiliwa na wajumbe wa mabaraza ya wilaya ya katiba baadaye mwezi huu hadi wa mwezi wa nane mwaka huu ambapo kupitia maoni ya mabaraza hayo, tume itakaa tena kuiboresha ili kupata rasimu kamili ya katiba mpya ambayo itapelekwa katika bunge la katiba kabla ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kura za maoni mwaka 2014.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: Joseph Axwesso Kutoka: Mbulu
06.06.2013 13:22
Napongeza tume ya kuandaa katiba mpya kwa kazi yao nzuri. Rasimu ya katiba ina mwelekeo wa democrasia zaidi na kuzingatia matakwa ya wananchi. Ni matumaini kuwa pamoja na mambo mengine Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete atakumbukwa na Watanzania.


Na: nasibu juma Kutoka: moshi
05.06.2013 08:56
iko vizuri ila ngependeza tungekua na serikali moja na pia napendekeza katiba mpya iweke wazi kuhusu masuala ya haki za wafanyakazi na mfumo wa elimu na suala la ardhi kwani migogoro mingi iko katika ardhi na masuala ya wafanya kazi namuomba mh Judge mstaafu Joseph Sinde Warioba aangalie masuala sugu ya kimahakama kama masuala ya ardhi na wafanyakazi na yapewe nafasi katika katiba mpya. kiukweli rasimu imejitaidi kuangalia mambo muhimu lakini suala la ardhi,elimu na wafanyakazi nalo lipewe nafasi kwa namna yake.KAZI NJEMA


Na: DENIS HITLER SANCHAWA Kutoka: MUGUMU, SERENGETI
05.06.2013 08:03
Swala la Mgombea binafsi pia litizamwe upya . Ifahamike kwamba katiba ikiruhusu Mgombea binafsi hapa hakuna umhimu wa vyama vya siasa . Pia, kuna uwezekano mkubwa wa nchi kuendeshwa na watu matajiri tu kwa kununua kura toka kwa watu masikini ambao nadhani ndo walio wengi.Hivyo napendekeza mgombea awe mwanachama wa chama cha siasa kianachotambulika au kilichosajiriwa na msajiri wa vyama vya siasa.


Na: DENIS HITLER SANCHAWA Kutoka: MUGUMU SERENGETI
05.06.2013 07:51
1. Napendekeza kuwepo na uhuru wa kitaaluma(academic freedom) katika katiba Mpya. Kwani mara nyingi nimeshuhudia wahadhiri wa vyuo vya elimu ya juu wanakosa uhuru wa kutoa maoni yao hasa mambo yanayohusu serikali kwa kile kinachosemekana kuwa wanafundisha siasa.
2.Napendekeza mawaziri wateuliwe on merit basis /kwa sifa. Kwa mfano,Mtu aliyesomea ualimu na akafanya kazi ya ualimu katika idara ya elimu nadhani anafaa kuwa Waziri wa Elimu. Aliyesomea sheria anafaa kuwa waziri wa sheria , kilimo na wizara zingine vilevile. Sifa za ziada pia zitizamwe has uzoefu na competency based
3.Swala la serikali tatu litizamwe upya. Wasiwasi wangu ni kwangu tunaweza kujikuta tunaongeza matatizo badala ya kusuluhisha tatizo. Moja kati ya hotuba ya Baba wa Taifa juu ya muungano '' alisema 1+1 lini ikawa 3? kama swala ni serikali tatu ipo siku watasema sisi Watanaganyika na Wao Wazanzibari, Sisi Wapemba na Wao Waunguja..........


Na: rashid said Kutoka: mwananchi
04.06.2013 16:41
Mambo ya muungano yabakie matatu tu.
1 katiba
2ulinzi na usalama
3 elimu ya juu


Na: Amir Faki Kutoka: Mwananchi
04.06.2013 16:37
Mambo ya muungano yabakie matatu tu
1 Ulinzi na usalama
2 Katiba
3 uraia


Na: nickson mutasingwa Kutoka: tanzania
04.06.2013 12:43
mimi nafikiri kuwa sasa umefika wakati ambao watanzania tunaanza kupata matumaini kuwa yale ambayo tumekuwa tukiyaona kwa watu wa mataifa mengine yanaanza kufanyiwa kazi nchini kwetu. Nafikiri kuwa huu ni mwanzo mzuri sana

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mafuriko Dar-es Salaam - VOA MItaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
16.04.2014 14:06
Karibu watu 10 wamefariki na maelfu kuharibiwa makazi yao jijini Dar es Salaam kufuatia mvua kali ya siku chache.