Jumatatu, Septemba 22, 2014 Local time: 14:12

Habari / Marekani

John Kerry aanza rasmi kazi yake.

Seneta wa zamani wa Massachusets na mwenyekiti wa zamani wa kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti  akiapishwa rasmi kuwa waziri wa mambo ya nje huku mke wake, Teresa Heinz Kerry akiangalia.
Seneta wa zamani wa Massachusets na mwenyekiti wa zamani wa kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti akiapishwa rasmi kuwa waziri wa mambo ya nje huku mke wake, Teresa Heinz Kerry akiangalia.
Waziri mpya wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amepiga simu zake za kwanza kwa viongozi wa nje akiwa kama mwanadiplomasia wa juu wa Marekani.
Wizara ya mambo ya nje inasema Kerry amempigia  simu waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas jumapili. Aliwaambia wote kuwa anaahidi kufuatilia binafsi suala la amani Mashariki ya Kati . Pia alisema maamuzi ya Israel kuachia faida ya kodi ni hatua nzuri.
Wizara ya mambo ya nje inasema Kerry aliwapigia mawaziri wa mambo ya nje wa Canada, Mexico na Uturuki  siku ya  Jumamosi. Pia amekutana na kuzungumza na kila waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani aliye hai akitaka ushauri wao.

John Kerry aliapishwa Ijumaa iliyopita kama waziri wa mambo ya nje kuchukua nafasi ya Hillary Clinton aliyeomba kustaafu baada ya kutumikia serikali ya Marekani kwa muda mrefu.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maudhui ya wavuvi wa Bagamoyo-VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
20.09.2014 15:14
Wafanyabiashara wa samaki katika wilaya ya Bagamoyo, Tanzania waelezea changamoto zinazowakabili katika biashara kuu ya uvuvi, miongoni mwao ukosefu wa soko na mahala ya kuhifadhi samaki wanaovua.