
Maandamano kupinga uchimbaji gesi Mtwara

Magari ya serikali yaliyochomwa moto Mtwara

Bango kuhusiana na mzozo wa gesi Mtwara

Nyumba yawaka moto Mtwara kufuatia maandamano dhidi ya kusafirisha gesi kutioka Mtwara hadi Dar es Salaam

Nyumba yawaka moto Mtwara

Polisi wakamata waandamanaji walosababisha vurugu Mtwara

Nyumba ya mbunge iliyovunjwa na waandamanaji Mtwara
Bunge la Tanzania limeunda kamati maalumu ya wabunge watakaokwenda mikoa ya kusini Mtwara na Lindi kutathmini mzozo wa gesi katika mikoa hiyo.
Spika wa bunge Anne Makinda amesema kamati hiyo itarejesha matokeo yatakayopatikana na baadae kujadiliwa katika baraza la bunge lililoanza Jumatatu.
Wakazi wa mtwara wanapinga Serikali ya Tanzania kutumia bomba kusafirisha gesi iliyogundulika mkoani humo kwenda Dar es salaam hali iliyozua ghasia na kusababisha maafa ya watu.
Hadi sasa Serikali ya Tanzania imesisitiza kuendelea na msimamo wake wa kusafirisha gesi hiyo . Tayari kuna vikao kadhaa vimefanywa ili kuona jinsi ya kutatua mzozo huo lakini hakuna mafanikio yoyote.
Hivi karibuni rais Jakaya Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari vya Tanzania akisema kuwa kama kila mkoa utagomea rasilimali zake basi nchi itapasuka vipandevipande hali iliyochechea tafrani.