Jumamosi, Mei 18, 2013 Local time: 06:55

Habari / Afrika

Hali ya utulivu yarejea huko Eritrea.

Rais wa  Eritrea  Isaias AfewerkiRais wa Eritrea Isaias Afewerki
x
Rais wa  Eritrea  Isaias Afewerki
Rais wa Eritrea Isaias Afewerki
ukubwa wa habari - +
Hali  ya utulivu  yaripotiwa kurejea tena huko Eritrea siku moja baada ya kundi la askari waasi kujaribu kuchukua wizara ya mambo ya habari ya nchi hiyo.
Zaidi ya askari waasi 100  walivamia wizara hiyo huko Asmara mapema Jumatatu na kuwaamrisha watangazaji wa habari wa Televisheni ya kitaifa kusoma taarifa ya kudai kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa na kusema katiba ya 1997 itaheshimiwa.
Haikujulikana mara moja jinsi gani hali hiyo ilivyotulizwa lakini wanajeshi hao inaaminika waliondoka wizarani hapo Jumatatu usiku.
Katika ujumbe uliotolewa kwenye mtandao wa  Twitter  Jumanne mkurugenzi wa ofisi ya rais wa Eritrea Yemane  Ghebremeskel amesema hali sasa ni tulivu.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--