Jumanne, Septemba 16, 2014 Local time: 07:22

Habari / Afrika

Marekani yamtaka Rais wa Misri kufuta usemi wake.

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

makala zinazohusiana

Marekani imemtaka rais wa Misri Mohamed Morsi kufuta usemi wake wa  maneno ya kichochezi  dhidi Waisrael aliyotoa kabla ya kuchaguliwa.

Kwa mujibu wa kipande cha habari kilichotolewa kwenye televisheni  wiki iliyopita na Middle East Media Research Institute,  mwaka 2010 bwana.Morsi aliwaelezea Waisraeli kama wavamizi wa  Palestina na pia kama wanyonya damu na wapenda vita  na kizazi cha  nguruwe na nyani.

Alitoa maneno mengine  yasiyo ya kweli na kuwataka raia wa Misri kuwafundisha watoto wao kuchukia wayahudi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Viktoria Nuland aliwaambia waandishi wa habari  jumanne kwamba Washington inalaani maneno yaliotolewa na rais Morsi.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mgomo wa Wafanyabiashara Dar es Salaam - VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
03.09.2014 16:46
Baadhi ya wafanyabiashara wa Dar es Salaam wamefanya mgomo kupinga utumiaji wa mashini za elektroniki zaa kutoa risiti, kuweza kupima mapato yao kwa ajili ya kodi EFD.