Alhamisi, Aprili 24, 2014 Local time: 23:55

Habari / Afrika

Majeshi ya Mali yapambana na wanamgambo wa Ansar Dine.

Wanamgambo wa kundi la  Ansar Dine wakiwa kwenye gari huko Gao kaskazini Mashariki mwa  Mali.Wanamgambo wa kundi la Ansar Dine wakiwa kwenye gari huko Gao kaskazini Mashariki mwa Mali.
x
Wanamgambo wa kundi la  Ansar Dine wakiwa kwenye gari huko Gao kaskazini Mashariki mwa  Mali.
Wanamgambo wa kundi la Ansar Dine wakiwa kwenye gari huko Gao kaskazini Mashariki mwa Mali.
ukubwa wa habari - +
Majeshi ya Mali yalipambana na wapiganaji wa kiislam wakati wanamgambo wakijaribu kwa mara ya pili wiki hii kuingia ndani zaidi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali ya Mali.
Afisa wa juu wa jeshi la  Mali akiongea kwa kwa misingi ya kutotajwa jina ameiambia VOA kwamba mapigano hayo yalitokea katika mji wa Kona, ambao upo karibu na eneo linalodhibitiwa na serikali kati kati ya nchi.
Mwandishi wa VOA katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo  karibu na mapigano alisema malori yaliojaa wapiganaji wa kiislam yaliondoka kuelekea uwanja wa mapambano baada ya ghasia kuripotiwa kumalizika jumatano usiku .
Msemaji wa Ansar  Dine moja ya makundi yanayopambana na serikali alikataa kuielezea VOA juu ya mipango yao kama wataingia zaidi upande wa kusini. 
Mpaka sasa jeshi limeweka wanamgambo wa kiislam nje kidogo ya Mopti, eneo lililo ngome ya serikali. Majeshi ya Mali yalipambana na wanamgambo katika eneo hilo wiki hii.

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mafuriko Dar-es Salaam - VOA MItaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
16.04.2014 14:06
Karibu watu 10 wamefariki na maelfu kuharibiwa makazi yao jijini Dar es Salaam kufuatia mvua kali ya siku chache.