Jumatatu, Februari 08, 2016 Local time: 17:16

  Habari / Afrika

  Wanaharakati walaumu watu kujichukulia sheria mkononi Congo.

  Waasi wa kundi la M23 wakibeba bidhaa karibu na mpaka wa Congo na Uganda huko Bunagana, DRC.Waasi wa kundi la M23 wakibeba bidhaa karibu na mpaka wa Congo na Uganda huko Bunagana, DRC.
  x
  Waasi wa kundi la M23 wakibeba bidhaa karibu na mpaka wa Congo na Uganda huko Bunagana, DRC.

  Huko jamhuri ya kidemokrasi ya Congo , wanaharakati wa makundi ya kijamii wanasema magenge yameua watu 9 wanaotuhumiwa kwa uhalifu katika mji wa mashariki wa Goma tangu mwezi Novemba. Wanaharakati hao wanalaumu ongezeko kwa kile  kinachoitwa  watu kujichukulia sheria mkononi  kwa vile serikali imeshindwa kuwasaka na kuwafunga zaidi ya wafungwa elfu moja mia moja waliokimbia jela.
  Mauaji holela si  kitu cha ajabu huko Goma, hata kabla ya kundi la waasi la M23 kuchukuwa udhibiti wa mji huo  mwezi Novemba, na baadae kuondoka mapema mwezi Desemba. Lakini tangu hapo viongozi wa makundi ya kiraia na wa serikali, wanasema kumekuwepo na ongezeko la idadi ya washukiwa wahalifu  kuuwawa na magenge.
  Jean Pascal Mugaruka ni kaimu mkuu wa kundi la kiraia kwa mji wa Goma
  anaiambia sauti ya America kuwa tangu mwishoni mwa Novemba, takriban watu 9 wamechomwa  moto wakiwa hai, kwa sababu walipatikana wakiiba au waligundulika  wakidhibiti mali iliyoibiwa.
  Kwa mujibu wa  Mugaruka, watu wamekuwa wakichukuwa sheria mikononi mwao kwa sababu mfumo wa sheria haufanyi kazi ipasavyo na wamekereka kuwa  zaidi ya wafungwa elfu moja mia moja waliachiliwa kutoka jela.
  Pia watu wamekuwa wakilipiza kisasi kwa unyanyasaji waliofanyiwa na waasi wa M23.
  Vyanzo kadhaa vimeiambia sauti ya America kwamba wafungwa katika jela kuu, waliachiliwa na wanajeshi hapo Novemba 20, kabla jeshi la Congo  kuondoka  Goma na kuwaachia  waasi.
  Karibu mwezi mzima wa  Desemba, jela hiyo ili haitumiki, lakini katika wiki mbili zilizopita, baadhi ya majengo yamefunguliwa tena.
  Anasema sasa jela inafanya kazi tena mjini  Goma, kwa hivyo watu kujichukulia sheria mikononi hakutastahmiliwa tena,  ingawaje mfumo wa sheria haufanyi kazi vilivyo, na mahakama za kijeshi bado hazijaanza tena  kufanya shughuli zake.
  Anasema makundi ya kiraia yamezungumza dhidi ya mauaji holela na yanapanga harakati za kuwaelimisha watu  dhidi ya vitendo hivyo.
  Makundi ya kiraia  mjini  Goma  yanaitaka serikali kuwasaka wafungwa waliotoroka, wengi wao ambao ni wanajeshi waliopatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha.
  Mugaruka anasema hadi sasa chini ya wafungwa 20, wamerudishwa kwenye jela kuu, lakini serikali bado inaendelea kuwasaka wengine.
  Anasema  jeshi la polisi  limeahidi  tuzo  ya dola mia moja kwa mtu yeyote atakayetowa maelezo yatakayopelekea kukamatwa kwa mfungwa aliyetoroka, na kwamba serikali pia wameandaa doria mchanganyiko za jeshi na polisi ambao wanawafuatilia majambazi, na  majambazi wengine wameuwawa.

  You May Like

  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.
  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.