Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:00

Ghasia za kingono dhidi ya wanawake zaongezeka Kenya.


Wanawake wa Kenya katika mkutano juu ya haki zao.
Wanawake wa Kenya katika mkutano juu ya haki zao.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema ghasia za kingono dhidi ya wasichana nchini Kenya zinaongezeka huku wengi wao wakishambuliwa na watu wasiowajua.

Madhavi Ashock mwakilishi wa Unicef nchini Kenya aliiambia Sauti ya Amerika kwamba watoto wako hatarini katika jumuiya zao, wakisema kwamba wengi wamekuwa wakishambuliwa wakati wakitembea kutoka na kuelekea shuleni.

Ashock anasema wakati mwingine mashambulizi hayo yanapelekea unyanyapaa kwenye jamii, magonjwa ya zinaa na mimba. Wakati mwingine hupelekea watoto hao kushindwa kuendelea na masomo.

Serikali ya Kenya inasema imedhamiria kumaliza vitendo hivyo dhidi ya watoto. Ahmed Hussein afisa katika wizara ya jinsia, watoto na maendeleo ya jamii anasema serikali iko katika mpango wa kutengeneza maeneo ya kulinda watoto nchi nzima ili kuweza kupambana na matukio ya ghasia na unyanyasaji. Amesema serikali imedhamiria kufanikisha mipango iliyopo kwenye ripoti hiyo.
XS
SM
MD
LG