Jumatatu, Machi 30, 2015 Local time: 15:53

Habari / Dunia

Obama amwonya rais Assad

Obama akitoa hotuba.
Obama akitoa hotuba.
Rais Barack Obama  amemwonya rais wa Syria  Bashar al-Assad kwamba atawajibishwa endapo majeshi yake yatatumia silaha za kemikali dhidi ya upinzani nchini Syria.
Bw. Obama alitamka hayo katika kikao hapa Washington  kusisitiza msimamo wa Marekani dhidi ya ulimbikizaji wa silaha za nuklia na kemikali wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya  mkataba wa ushirikiano wa kupunguza vitisho vya silaha za kemikali kati ya Marekani na Russia.

Lakini  kilichogonga vichwa vya habari  ni onyo lake kwa rais wa Syria, siku moja baada ya Washington kuionya  Damascus  dhidi ya matumizi ya silaha za kemikali. Bw. Obama alisema Marekani itaendelea kuunga mkono azma halali ya raia wa Syria, na kutoa misaada ya kibinadamu kwa upinzani na katika makabidhiano huru ya madaraka pasipo utawala wa Assad. 

Alimwonya  rais Assad kuwa dunia inatizama kinachoendelea nchini Syria na kwamba matumizi ya silaha za kemikali kamwe hayatakubalika. Na ikiwa atafanya kosa  la kutumia silaha hizo kutatokea madhara na Assad atawajibika.

Bwana  Obama alisisitiza kuwa dunia haiwezi kuruhusu  karne ya 21 kutumbukizwa katika kiza cha karne ya 20 ya matumizi ya silaha  kama hizo. Alisema jukumu la kuzuia  ugaidi wa kutumia silaha za nuklia ni mojawapo ya maswala yaliyopewa  kipaumbele kwa usalama wa kitaifa , na kwamba dunia inasogea mbele kuhakikisha  hakuna silaha za nuklia katika siku za usoni.
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Waandamana kupinga ubakaji Kenyai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
27.03.2015 18:06
Mamia ya wanawake nchini Kenya hivi majuzi walishiriki maandamano kupinga vitendo vya ubakaji ambayo vimekithiri nchini humo