Jumapili, Januari 25, 2015 Local time: 21:13

Habari / Afrika

Waasi wa M23 waondoka kwenye miji waliyoteka DRC.

Wanajeshi waasi wa M23 wakiwa kaskazini mwa Goma.Wanajeshi waasi wa M23 wakiwa kaskazini mwa Goma.
x
Wanajeshi waasi wa M23 wakiwa kaskazini mwa Goma.
Wanajeshi waasi wa M23 wakiwa kaskazini mwa Goma.
Wakazi wa mji wa Sake ashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wanasema wanajeshi waasi wa kundi la M23 wamevamia nyumba na kuiba pesa kutoka kwa wafanyabiashara wakati wanajiandaa kuondoka katika eneo hilo.

Pembeni mwa barabara kwenye mji wa Sake nje ya eneo ambalo kundi la M23 linalinda kituo cha ukaguzi, kundi na wakazi wanalalamika kuhusu magenge ya waasi waliouvamia mji  wakati wa usiku.

Mkazi mmoja aliyekataa kusema jina lake alionesha madirisha mawili yaliyoharibiwa katika nyumba yake ambayo anasema wanajeshi walivunja kwa kutumia bunduki zao wakati familia yake ikila chakula cha jioni.

Anasema waliingia ndani ya nyumba hiyo saa saba usiku . Walichukua pesa magodoro na kila kitu, walipoamka asubuhi hawakukuta kitu.

Katika makutano makuu ya barabara mjini humo,  madereva wa magari makubwa wamesimama pembeni mwa magari yao. Wanasema waasi wamewataka walipe  dola 320 ili waweze kuondoka mjini  na hawawezi kwenda popote mpaka wapate pesa.

Waasi walichukua udhibiti wa mji wiki iliyopita baada ya mapigano makali na jeshi la congo.

Lakini sasa kama sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na kundi la M23 na jeshi la Congo waasi wanajiandaa kuondoka kwenye mji wa Sake na mji ulio karibu wa Goma.
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Tatizo la maji, Pwani, Tanzaniai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
20.01.2015 18:50
Tatizo la maji safi linavyohangaisha wananchi katika maeneo ya mkoa wa Pwani, Tanzania. Vijiji hivi viko chini ya maili 50 tu kutoka mji mkubwa wa biashara, Dar es Salaam.