Jumapili, Mei 24, 2015 Local time: 16:02

Habari / Afrika

Museveni na Kagame hawatokubali serikali yeyote kupinduliwa na kundi la waasi

M23 rebels assemble police in Goma
M23 rebels assemble police in Goma
Viongozi wa Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sauti moja wamelitaka kundi la waasi la M23 lililouteka mji wa Goma siku ya Jumatatu usiku, kuondoka nmjini humo na hawatokubali mapinduzi dhidi ya serikali yeyote ya kanda ya maziwa makuu.

Rais Museveni wa Uganda akiuliza watafanya nini ikiwa kundi litakata kuondoka alisema "wataona chamtema kuni".

Museveni akutana na Kabila na Kagame
Museveni akutana na Kabila na Kagamei
|| 0:00:00
...    
🔇
X


Marais Yoweri Museveni, Paul Kagame na Joseph Kabila walizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo yao na kueleza kwamba ingawa wapiganaji wa M23 wanamadai yaliyo ya haki lakini hawawezi kutumia nguvu kupindua serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Rais Kabila amesema yuko tayari kuyasikiliza malalamiko ya waasi na atafanya kila awezalo kuyashughulikia.

Kwa Upande wake rais Kagame amesema kuhudhuria kwake mazungumzo hayo kunamaanisha anataka amani kwa kanda nzima, bila ya kutilia maanani sula la waandishi habari ikiwa anawaunga mkono wapiganaji wa M23.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: Kwame Edrick Kapinga Kutoka: Dodoma Tanzania
22.11.2012 20:37
Ni habari njema sana kusikia Rais Kagame na Museveni kutoa matamshi haya kutoka vinywa vyao.Ukirudi nyuma kuona wazi kwamba nchi zao ndizo nchi zinazoshutumiiwa na dunia kuwasaidia M23.
Lakini ni maneno ambayo lazima yachukuliwe kwa umakini na tahadhali kubwa sana.M23 wako goma na ni ngumu kwao kurudi nyuma dhahiri.Watoto wanawake wanateseka sana.Hawa ndio wahanga wakubwa sana.
Ni wakati sasa kwa ulimwengu kuchukulia swala hili ka ukubwa wa kipekee.


Na: Jafari selemani Mgendegen Kutoka: sinza DSM
22.11.2012 03:10
Hii ndio kauli tuliyokua tunaisubiria kwa hamu juu ya kuimalisha ulinzi katika nchi za kanda ya ziwa..kwa umoja tunaweza shinda waasi wenye uchu wa madaraka na vibaraka wa nchi za magharibi.
Mungu ilinde Afrika na machafuko.

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.