Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:27

CCM na CHADEMA wajiimarisha kwa uchaguzi mkuu ujao 2015


wafuasi wa chama tawala cha CCM Tanzania wakimaliza kampeni za uchaguzi wa 2010.
wafuasi wa chama tawala cha CCM Tanzania wakimaliza kampeni za uchaguzi wa 2010.
Vyama vilivyo na upinzani mkubwa kwa sasa nchini Tanzania, chama tawala CCM na chama cha upinzani cha demokrasia na maendeleo CHADEMA vimeanza kupigana vikumbo katika operesheni mbalimbali zinazolenga kujiimarisha kwa wananchi kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Wakati CCM kikionekana kama kuzinduka sasa na kutamngaza mkkati kabambe wa kujiimarisha baada ya kumalizika kwa mkutano wake mkuu na kupata safu mpya ya uongozi, CHADEMA kimetangaza kuendelea na operesheni yake ya mabadiliko hivi sasa wakija pia na mkakati mwingine wa kuimarisha uwezo wa viongozi wake.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye amesema sekretarieti mpya ya chama hicho ikiongozwa na katibu mkuu Abdulrahman Kinana pamoja na baadhi ya wa mawaziri watafanya ziara katika mikoa mbalimbali kwa lengo la kujiimarisha.

Nape amesema chama kitaongeza nguvu zaidi katika kusimamia utendaji kazi wa serikali na watendaji wake na ikibidi kuwawajibisha iwapo utendaji kazi wao hautakuwa wa kuridhisha badala ya kusubiri vyombo vingine vya dola.

Miongoni mwa mambo yaliyoamuliwa katika mkutano mkuu wa CCM uliomalizika hivi karibuni ni pamoja na chama kusimamia na kuisaidia serikali kutekeleza ahadi ambazo chama kilitoa kwa wananchi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita kupitia ilani yake ya uchaguzi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:10 0:00
Kiungo cha moja kwa moja



Wakati CCM ikitangaza ziara hiyo, Chadema kupitia Mkurugenzi wa Mafunzo na Organaizesheni wa chama hicho Benson Kigaila kimetangaza mkakati mwingine wa kujiimarisha kuanzia ngazi ya mtaa mpaka taifa kwa kufanya mafunzo kwa wenyeviti na makatibu wa kata na mikoa nchi nzima pamoja na Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mikakati ya vuguvugu la mabadiliko M4C..

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajenga makada wa chama hicho ktk kueneza sera za chama nchi nzima ambapo makada hao baadae watafanya mikutano ya ndani na mikutano ya hadhara ikiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi dhana ya mabadiliko.

Aidha chama hicho kimesema kitaendelea na mikutano yake ya hadhara ya M4 Change kuanzia Februari mwakani ambayo wataifanya nchini kote .

CCM wanajigamba kwamba sasa inataka kusukuma zaidi utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Hata hivyo Chadema imeuponda mkakati huo pamoja safu hiyo ya sekretari mpya ya CCM kwamba haitakuwa na jambo lolote jipya la kuwaeleza watanzania ikiwa haitawawajibisha watu wote waliotajwa na CHADEMA katika orodha ya mafisadi
XS
SM
MD
LG