Jumatano, Mei 22, 2013 Local time: 09:01

Habari / Afrika

Upinzani unasema utashinda uchaguzi Sierra Leone.

Waunga mkono wa chama cha  Sierra Leone People's Party (SLPP) wakiandamana kati ya mji wa Freetown na bango la mgombea wao Julius Maada Bio na mgombea mwenza Dr. Kadi Sesay.
Waunga mkono wa chama cha Sierra Leone People's Party (SLPP) wakiandamana kati ya mji wa Freetown na bango la mgombea wao Julius Maada Bio na mgombea mwenza Dr. Kadi Sesay.
ukubwa wa habari - +
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani huko Sierra Leone, John Benjamin anasema ana imani chama chake kitashinda katika uchaguzi wa rais utakaofanyika Jumamosi, kama ukiwa wa huru na haki.

Katika mahojiano na VOA Benjamin mwenyekiti wa chama cha Sierra Leone Peoples Party, SLPP,  anatabiri kwamba wapiga kura watakikimbia chama tawala cha All Peoples Congress kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Benjamin pia amesema ana matumaini uchaguzi utakuwa wa huru na haki Amesema ametiwa moyo kutokana na  kuwepo kwa wafuatiliaji wa kimataifa ambao wanaweza kufanya kuwa vigumu zaidi kwa mtu yeyote kufanya ghasia wakati wa uchaguzi.

Mgombea wa SLPP Julius Maada Bio ni mmoja kati ya  wagombea wanane wanaoshindana na  rais aliyeko madarakani Ernest Bai Koroma.

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--