Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:42

Wamarekani wapiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkubwa


Voters at their voting machines at the Utah State Capitol Tuesday, Nov. 6, 2012, in Salt Lake City.
Voters at their voting machines at the Utah State Capitol Tuesday, Nov. 6, 2012, in Salt Lake City.
Uchunguzi wa maoni ya uchaguzi wa Rais, siku moja kabla ya upigaji kura unaonesha Rais Barack Obama na mpinzani wake Gavana Mitt Romney wako sare asilimia 49 kwa asilimia 49. Hivyo wachambuzi wanasema mshindi wa uchaguzi huu ataamuliwa kutokana na kura za wajumbe wa Baraza la Majimbo.

Mobhare Matinyi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Washington anasema huwenda hata wagombea hao wakatokea sare kwa kupata kura sawa za wajumbe wa baraza la majimbo ambapo kuna wajumbe 538.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:22 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Anasema hali hiyo ikijitokeza basi itakuwa ni juu ya bunge jipya kumchagua Rais na Makamu Rais. Katika uchaguzi wa rais wa Marekani mgombea anahitaji kupata kura 270 za wajumbe wa majimbo ili kuweza kuchukua madaraka.

Bwana Matinyi anasema, wagombea wakipata kura 269 kila mmoja basi Baraza la Wawakilishi linamchagua rais na Baraza la Senet linamchagua Makamu Rais.Kuna uwezekano wa kuwepo na Rais wa chama kimoja na Makamu Rais kutoka chama kingine kwa kutegemea chama gani kinadhibiti mabaraza hayo mawili.



Upigaji kura ukiwa unaendelea katika majengo ya shule, makanisha na vituo vya zima moto, wagombea wa kiti cha rais waliendelea na kampeni za kuwahamasisha wapiga kura kwenda kupiga kura zao kwani matokeo ya uchaguzi huu utategemea ni chama gani kwa hakika kinafanikiwa kuwavutia wafuasi wao kupiga kura.
XS
SM
MD
LG