Alhamisi, Novemba 26, 2015 Local time: 06:16

Habari

Klabu ya waandishi wa habari Iringa yasitisha ushirikiano na polisi.

Mmoja wa makamishna wa jeshi la polisi nchini Tanzania.Mmoja wa makamishna wa jeshi la polisi nchini Tanzania.
x
Mmoja wa makamishna wa jeshi la polisi nchini Tanzania.
Mmoja wa makamishna wa jeshi la polisi nchini Tanzania.
Klabu ya waandishi wa habari mkoani  Iringa –IPC nchini Tanzania, kwa kushirikiana na waandishi wote wanaofanya kazi mkoani  humo,  kuanzia Jumanne imetangaza kusitisha ushirikiano wa kikazi baina yao na jeshi la polisi mpaka pale taarifa au majibu sahihi kutoka vyombo huru zitakapotolewa kujua aliyemuuwa mwandishi wenzao Daudi Mwangosi wakati wa vurugu za chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema na polisi.
 
Kazi hizo ni pamoja na kuwataarifu waandishi wote kuacha kwenda katika ofisi ya kamanda wa polisi kupata taarifa za matukio mbalimbali .
 
Mwangosi ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Chanel Ten alifariki Jumatatu majira ya saa 10 jioni  baada ya kupigwa na kile kinachosadikiwa kuwa bomu katika vurugu za wafuasi wa Chadema waliokuwa wakitawanywa na polisi.
 
Kumezuka utata wa nani anahusika na tukio hilo huku jeshi la polisi likitoa taarifa jumanne kusema uchunguzi wake unaonesha kuwa bomu lililompiga mwandishi Mwangosi lilitoka upande wa Chadema.

You May Like

Papa aendelea na ziara Afrika

Tunamatumaini kwamba ziara ya papa itaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa mioyo ya watu wa jamhuri ya afrika ya kati, ambayo itapelekea kurejea Amani na kurejea kwa waislamu na wakristo kuishi pamoja. Hili litapelekea maendeleo ya taifa. Zaidi

video VOA60 AFRIKA: NOVEMBER 25, 2015

wakimbizi nchini Djibouti waendelea kuvuka ghuba ya Aden kutoka Yemen, wakitoroka mizozo na mashmabulizi Zaidi

video Maoni ya Papa Francis yanayotofautiana na Waafrika

Muelekeo wa Papa Francis wa kufanya mabadiliko muhuimu katika Kanisa lam Katholiki yanatofautiana kwa kiwango fulani na maoni ya waumini wa kiafrika. Zaidi

sauti Zanzibar: Vikao vingi bila suluhisho

Vikao vinne tayari vimefanyika katika Ikulu ya Zanzibar na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wakiwemo wa zamani na wa sasa tangu kuzuka kwa mzozo wa matokeo ya uchaguzi lakini hakuna tamko rasmi mpaka sasa. Zaidi