Jumapili, Mei 19, 2013 Local time: 20:22

Habari / Afrika

Mabaki ya helikopta ya Uganda yapatikana Kenya

Juhudi za kuwatatuta wanajeshi saba wa Uganda wanaodhaniwa wamenusurika na ajali ya helikopta ziliendelea Jumanne huko mlima Kenya

Chris Kasaija, afisa wa cheo cha juu wa jeshi la anga la Uganda aokolewa mjini Nanyuki
Chris Kasaija, afisa wa cheo cha juu wa jeshi la anga la Uganda aokolewa mjini Nanyuki

Multimedia

Audio
ukubwa wa habari - +
Timu za waokozi Kenya wanasema wamepata miili ya wanajeshi wawili wa Uganda walofariki katika ajali ya helikopta ya jeshi la Uganda karibu na Mlima Kenya Jumapili usiku.

Simon Gitau, naibu mkuu katika idara ya mbuga ya kitaifa ya Mt. Kenya  amesema timu ya waokozi ilipata maiti mbili nje ya helikopta hiyo ambayo ilikuwa bado inaungua moto  Jumanne na kwamba kuna uwezekano  wa kupata maiti nyingine ndani ya helikopta hiyo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika msemaji wa wizara ya Ulinzi nchini Kenya Bogita Ongeri, anasema wameshapata helikopta zote tatu zilizoanguka wamezipata, na juhudi zinaendelea kuwatafuta wanajeshi watano ambao hawajajulikana walipo.

Mahojiano na Bogita Ongeri
Loading
12:00:00 / -:--:--

.

Alisema wanajeshi wengine watano waliokuwa kwenye helikopta nyingine ya jeshi la Uganda wamepatikana wakiwa hai. Maafisa wanasema wapelelezi wanadhani kuwa hali mbaya ya hewa  ndiyo iliyosababisha ajali za helikopta nne za jeshi la Uganda huko Kenya.

Helikopta hizo zilikuwa njiani kuungana na kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Afrika kwa mapigano dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia . Helikopta moja ilitua salama katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: Nehemiah Okonu Kutoka: Kitale Kenya
15.08.2012 08:32
Inasikitisha sana ndege zote tatu zillianguka.Je ni hali ya anga iliyofanya au zilikuwa na hitilafu?

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--