Jumatano, Mei 22, 2013 Local time: 03:33

Habari

Mwandishi wa habari wa Somalia auwawa

Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini SomaliaWanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
x
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
ukubwa wa habari - +
Watu wenye silaha wamemuuwa mwandishi wa habari maarufu wa Somalia eneo ambalo limekuwa hatari kwa watu wenye taaluma hiyo duniani.

Watu wasiojulikana jana walimuuwa kwa risasi Yusuf  Ali Osman anayejulikana  sana kwa jina la farey katika wilaya ya dharkenely mjini Mogadishu .

Osman mkurugenzi wa zamani  wa radio Mogadishu alikuwa anafanya kazi katika wizara ya habari ya somalia.

Jumuiya ya waandishi wa habari wa somalia iliyoko uhamishoni nchini Kenya imesema Osman ni mwandishi wa habari wa nane kuuwawa nchini somalia mwaka huu. katika taarifa jumuiya hiyo imesema inaumiza na kuvunja moyo kumpoteza mwandishi wa habari mahiri kila mwezi.

Mwakilishi maalumu wa umoja wa mataifa  kwa ajili ya somalia Augustine Mahiga alilaani kuuwawa  kwa Osman na kutoa mwito tena kwa maafisa wa somalia kufanya uchunguzi wa mashambulizi kwa waandishi wa habari.

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--