Jumatano, Machi 04, 2015 Local time: 11:30

Habari / Afrika

Kiprotich wa Uganda ashangaza dunia kushinda marathon London

Wanariadha katika mbio za marathon wakikimbia kupita mbele ya soko la Leadenhall, London
Wanariadha katika mbio za marathon wakikimbia kupita mbele ya soko la Leadenhall, London
Uganda yajinyakulia medali ya kwanza kabisaya dhahabu katika mbio za marathon katika mashindano ya Olimpiki Junmapili, kutokana na ushindi wa Steven Kiprotich, aliyewashinda wakenya wawili katika dakika za mwisho za mbio hizo mjini London.

Huu ni ushindi mwingine katika michezo ya Olimpiki mwaka huu ambao mashabiki na watalamu wa riadha hawakutatazamia. Kiprotich aliwashinda Wakenya wawili Abel Kirui na Wilson Kipsang, walokuwa wakiongoza kwa muda mrefu katika dakika za mwisho na kushinda mbio kwa kutumia saa 2, dakika 8 sekunde 1.

Wakenya walimaliza mbio hizo kwa kumkumbuka mwenzao marhemu Sammy Wanjiru. Miaka minne iliyopita wanjiru alinyakua dhahabu ya kwanza ya Kenya katika mbio za marathon huko Berjing na alifariki mwaka jana baada ya kuanguka kutoka nyumba ya ghorofa kutokana na ugomvi wa nyumbani.

Wakenya hawana la kusema

Matokeo ya Jumamosi na Jumapili katika riadha yamewasababisha watu wengi kujiuliza imekuwaje Wakenya hawakuweza kufua dafu katika mbio zote ambazo walitarajiwa kuwika kama kawaida yao.

Mchambuzi wa masuala ya riadha Peter Njenga huko Nairobi anasema matokeo ni ya kusikitisha lakini ndiyo hali ya michezo. Anasema hiui yote inatokana na kutojitayarisha vyema wanariadha na mivutano kati yao na maafisa wao.

Uchambuzi wa Peter Njenga
Uchambuzi wa Peter Njengai
|| 0:00:00
...    
🔇
XKwani Jumamosi katika mbio za mita 5 000 Mo Farah wa Uingereza alijinyakulia dhahabu yake ya pili kwa kutumia muda wa dakika 13, sekunde 41, nukta 31 akifuatwa na Dejen Genremeskel wa Ethopia na Mkenya Thomas Longosiwa.

Medali nyingine ya dhahabu ambayo Wakenya walitarajiwa kushinda na wakaipoteza  ni katika mbio za mita 800 wanawake, ambapo bingwa mtetezi Pamela  Jelimo, aliondoka matupu alipotokea wanne.

Mshindi wa mbio hizo alikua ni bingwa wa dunia Mrusi Mariya Savinova aliyemshinda pia Muafrika Kusini Caster Semenya aliyelazimika kuridhika na medali ya fedha.
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Wakenya watoa maoni kuhusu mfumo wa dijitalii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
26.02.2015 19:55
Tangu uamuzi wa serikali kuondoa matangazo ya analog Wakenya wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mfumo huo na kuzimwa kwa baadhi ya matangazo ya mashirika makuu ya televisheni Kenya