Alhamisi, Juni 20, 2013 Local time: 06:30

Habari / Afrika

Viongozi wa Afrika hawajakubaliana juu ya Congo

Viongozi wa mataifa ya kanda ya Maziwa Makuu wakutana Kampala
Viongozi wa mataifa ya kanda ya Maziwa Makuu wakutana Kampala
ukubwa wa habari - +
Viongozi walitangaza Jumatano baada ya kukutana Kampala kwamba wameweza kukubaliana juu ya haja ya kupaleka kikosi cha kimataifa kupambana na makundi ya waasi huko mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Hata hivyo, katika taarifa yao ya mwisho viongozi hao hawakutaja kutokubaliana kwao juu ya namna ya kuundwa kwa kikosi hicho ingawa wameeleza haja ya kuushinda uwasi huo kwa haraka iwezekanavyo.
Ripoti ya Saleh Mwanamilongo
Loading
12:00:00 / -:--:--


Rais wa Uganda Yowerei Museveni alisema viongozi hao wamekubaliana kukutana katika muda wa mwezi mmoja unaokuja baada ya mawaziri wa ulinzi wa mataifa manane kukutana na  kutayarisha mipango yote ya kuundwa kwa kikosi hicho  katika muda wa wiki mbili zijazo.

Tofauti kubwa iliyojitokeza kwenye mkutano huo ni msimamo inayotofautiana kati ya Kongo na Rwanda.Serikali ya Kinshasa inapenmdelea kuwepo na kikosi cha kimataifa kisichopendelea upande wowote kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, huku Kigali inapendelea kikosi cha kikanda, kipelekwe ndani ya Jimbo la Kivu. 
 
Wimbi la ghasia nchini DRC lilianza Aprili, wakati wanajeshi kutoka jeshi la taifa kuasi na kuunda kundi la waasi  la M23. Tangu wakati huo, mapigano katika jimbo la Kivu ya Kaskazini yamesababisha maelfu ya watu kukimbilia mpakani na  kuingia nchi jirani ya Uganda.
Katika mkutano na waandishi wa habari Afrika Kusini  Jumanne, waziri wa mambo ya nchi ya nje Marekani, Bi Clinton alitoa wito kwa viongozi  kanda hiyo ya wa Maziwa Makuu, kufanya kazi pamoja kukomesha vurugu katika mashariki ya Kongo.

“Uamuzi wa Uganda Rwanda na DRC kuanza tena mazungumzo ni hatua muhimu. Kumekuwa na ongezeko la ghasia, ubakaji, mauaji, na ukiukaji mbaya wa haki za binadamu katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita iliyokuwa inafanywa na makundi ya wahuni na waasi. Na tunaunga mkono juhudi za DRC na tunazihimiza nchi zote katika kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Rwanda kufanya kazi pamoja ili kukata msaada kwa waasi wa M23 na kuwanyanganya silaha na kuwafikisha mahakamani viongozi wao.”

Wote marais wa Kongo Joseph Kabila na Paul Kagame wa Rwanda  walihudhuria mkutano wa Kampala, ambao ulikuwa na  lengo la kupunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili. 

Baada ya mkutano huo, waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Uganda  Oryem Okello aliwambia waandishi habari kwamba  makubaliano hayo ni ishara kwamba marais Kabila na Kagame wako tayari kushirikiana.

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--