Jumanne, Mei 21, 2013 Local time: 10:21

Habari

Clinton azungumza na maafisa wa Misri

Waziri Hillary Clinton azungumza na Mohammed Tantawi

Rais wa Misri Mohammed Morsi
Rais wa Misri Mohammed Morsi
ukubwa wa habari - +

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amekutana leo mjini Cairo na mwanajeshi wa ngazi ya juu wa Misri Mohammed Hussein Tantawi siku moja baada ya kufanya mazungumzo na rais mpya nchini humo Mohammed Morsi.  Clinton alisema Field Marshal Tantawi ambaye alikuwa kaimu kiongozi  baada ya kutimuliwa madarakani kwa rais Hosni Mubarak, alijadilia maswala pana likiwemo swala  la mchakato wa  kisiasa, umuhimu wa kulinda haki za Wamisri wote na uthabiti wa kikanda. Clinton pia amezungumza na viongozi makundi ya kina mama na wale wa dini ya Kikristo  kabla ya kuelekea mji wa Alexandria kwa sherehe za kupeperusha bendera ya Marekani katika ofisi ya kibalozi mjini humo. Ataondoka Misri baaadye Jumapili kuelekea Israel.

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--