Jumanne, Februari 09, 2016 Local time: 18:45

  Habari

  Viongozi wa Afrika wazindua ofisi za kupambana na Malaria

  Mwaka 2009 katika mkutano wa umoja wa Afrika viongozi walikubaliana kuanzisha ushirikiano huo.

  Mbu anayeambukiza malaria
  Mbu anayeambukiza malaria
  Dinah Chahali

  Ushirikiano wa viongozi wa Afrika katika kupambana na ugonjwa wa mara katika bara la Afrika – Alma, umefungua njia ya kuwezesha nchi za afrika kupambana na ugonjwa huo kwa nguvu moja.

  Rais wa Liberia Elen Johnson Sir – Leaf aliyoko ziarani nchini Tanzania ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Alma pamoja na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete aliyemuachia uenyekiti huo leo jijini Dar es salaam wamezindua ofisi za sekretariet ya ushirikiano huo ya viongozi wa Afrika ya kupambana na malaria .

  Katika uzinduzi huo rais Kikwete alisema asilimia 89 ya vifo vinavyotokana na malaria duniani kote vinatokea Afrika vivyo akasema ni budi kuunganisha nguvu pamoja ili kutafuta misaada kupambana na ugonjwa huo.

  Mwaka 2009 katika mkutano wa umoja wa Afrika viongozi walikubaliana kuanzisha ushirikiano huo.

  Kwa mujibu wa marais hao kimsingi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita kiwango cha malaria kimepungua kwa asilimia 33 hatua ambayo ni mafanikio kwa chombo hicho.

  Hata hivyo rais wa Liberia ametaka asilimia 15 ya  kwenye mapato ya nchi hizi kuelekezwa katika sekta ya afya hususan ugonjwa wa malaria kama iliovyoadhimiwa kwenye malengo ya kuadhimishwa ushirikiano huo huko Abuja nchini Nigeria.

  You May Like

  Umoja wa Mataifa waonya kwamba wasichana wengi hatarini kufanyiwa ukeketaji.

  Baadhi ya wanawake wanafariki dunia kutokana na kitendo hicho. Zaidi

  Zimbabwe yatoa wito wa msaada zaidi kusaidia kukabiliana na ukame

  Zimbabwe ina takriban watu millioni 2.5 wanaokabiliwa na njaa , na inalaumu mfumo wa hali ya hewa ujulikanoa kama El Nino kwa kusababisha ukame mbaya huko Kusini mwa Afrika Zaidi

  sauti Wachambuzi waonya kuhusu mzozo wa Zanzibar

  Wadadisi wanasema kwamba mvutano huo utamalizwa na Wazanzibari wenyewe. Zaidi

  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.