Jumanne, Desemba 01, 2015 Local time: 08:36

Habari

Al-Shabab yatishia kuendeleza mashambulizi Afrika Mashariki

Kundi la waasi nchini Somalia, Al-Shabab lenye uhusiano na mtandao wa Al Qaida ladai kuhusika na mashambulizi ya Jumapili nchini Uganda.

Khadija Riyami

Kiongozi wa kundi la kigaidi  nchini Somalia lenye uhusiano na Al Qaida amedai kuhusika na mashambulizi ya mabomu ya Jumapili nchini Uganda na kusema anapanga mashambulizi zaidi.
Onyo limetolewa na Sheik Muktar Abu Zubayr na kutangazwa kwenye vituo vya radio hivi leo Alhamisi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Amesema  kundi lake la Al Shabab litaendelea kulipiza kisasi dhidi ya waganda kwa kushiriki katika jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Mabomu ya Jumapili yameua zaidi ya watu 70 waliokuwa wakiangalia fainali za kombe la dunia kwenye televisheni mjini Kampala.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameapa kujibu vikali. Amesema wanajeshi wa Uganda nchini Somalia walikuwa  mpaka hivi sasa wakishughulika na shughuli za ulinzi, lakini wataanza kulivunja kundi la Al Shabab. Uganda ilitangaza mapema hivi leo kwamba itapeleka wanajeshi elfu mbili zaidi nchini Somalia.
Al Shabab na makundi mengine ya wanamgambo yamekuwa yakipigana kwa zaidi ya miaka mitatu kuchukua udhibiti wa Somalia. Lakini mabomu ya Kampala yalikuwa ni mashambulizi ya kwanza makubwa ya kigaidi  nje ya Somalia.
Maafisa wa Uganda wanasema wamewakamaa  raia wanne wa kigeni kuhusiana na fulana ya kujitoa mhanga ambayo haikulipuka iliyogunduliwa kwenye la tatu karibu na Kampala. Hawakutaja utaifa wa wale waliokamatwa, lakini Negussie Balcha, mkuu wa taasisi inayojulikana kama Ethiopian Community in Uganda ameiambia sauti ya Amerika – VOA – kwamba raia wanne wa Ethiopia wametiwa mbaroni.

You May Like

Mashambulizi ya Waasi wa ADF yasababisha vifo Mashariki mwa DRC

Afisa wa Umoja wa Mataifa nchini DRC asema waasi wa ADf watawajibishwa kwa vitendo vyao vya kihalifu na mauaji. Zaidi

Hatua zaidi zahimizwa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Obama alisema ameshuhudia binafsi athari za mabadiliko ya hali ya hewa huko Alaska, ambako theluji kubwa kubwa inaanza kuyayuka, momonyoko wa maeneo ya Pwani na vijiji vinazama baharini. Zaidi

video VOA60 AFRIKA November 30, 2015

Papa Francis amaliza ziara yake nchini C.A.R, kwa kutowa wito wa kuwepo amani na maridhiano baina ya waislamu na wakristo. Zaidi

Kenya Teens, LGBT Face Challenges Seeking HIV Care

AIDS is the leading cause of death among adolescents in Kenya and throughout Africa Zaidi

Ministry: 2 Kenyans With Alleged Iran Links Arrested for Plotting Attacks

Interior Ministry says two Kenyans plotted attacks, whose targets included 'hotels in Nairobi frequented by Western tourists and diplomats' Zaidi

mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one