Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:51

Al-Shabab yashambulia maafisa wa serikali Somalia


Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab la nchini Somalia

Maafisa nchini Somalia wanasema Naibu Waziri Mkuu nchini humo alijeruhiwa na watu wengine wasiopungua 10 waliuwawa katika shambulizi lililofanywa na wanamgambo wa kundi la al-Shabab kwenye hoteli moja katika mji mkuu, Mogadishu.

Mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika-VOA- mjini Mogadishu alisema mlipuko wa kwanza ulitokea muda mfupi baada ya wageni kumaliza kusali sala ya Ijumaa kwenye jengo la Central Hotel karibu na ukumbi wa National Theatre. Mlipuko wa pili ulifuatia na kisha milio ya risasi.

Msemaji wa mashirika ya usalama, Qasin Ahmed Roble alisema gari moja lililojaa milipuko liliingia ndani ya hoteli wakati wa sala ya Ijumaa. “Tunachunguza nani alitegua milipuko ya kwenye gari na ni kwa njia ipi. Tunawahoji walinzi wa hoteli alisema”.

Mashirika ya usalama yakiwa nje ya jengo la Central Hotel
Mashirika ya usalama yakiwa nje ya jengo la Central Hotel

Moshi mzito mweusi ulionekana ukivuma kutoka jengo la Central Hotel ambalo ni maarufu kufikiwa na maafisa ikiwemo wabunge na mawaziri wa serikali. Maafisa walisema Naibu Meya wa mji wa Mogadishu, Mohamed Aden Guled alikuwa ni miongoni mwa watu waliokufa katika shambulizi hilo. Miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu, Mohamed Omar Arte na Waziri wa Usafiri na masuala ya anga, Ali Ahmed Jama Jangali.

Wakati huo huo Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud alilaani shambulizi hilo kupitia mtandao wa Twitter akisema tukio hilo halikubaliki na akisema anawaombea wale wote waliokumbwa na mkasa huo.

Kundi la wanamgambo wa Al-Shabab linadai kuhusika katika shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG