Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:29

Pembe za ndovu zakamatwa Kenya.


Shirika la wanyama pori Kenya lasema msako unaendelea dhidi ya wamiliki wa pembe za ndovu Mombasa.
Shirika la wanyama pori Kenya lasema msako unaendelea dhidi ya wamiliki wa pembe za ndovu Mombasa.
Serikali ya Kenya imeimarisha vita dhidi ya wawindaji haramu, kutokana na visa vya wanyama-pori kuuwawa.

Katika kisa cha hivi karibuni Polisi wa Kenya kwa ushirikiano na maafisa wa idara ya forodha mjini Mombasa, wamekamata shehena ya pembe za ndovu zilizokuwa zikisafirishwa kutoka nchini Uganda kuelekea Malaysia.

Naibu kamishna wa idara ya forodha nchini Kenya John Changole amesema vifurushi sabini vya pembe vilikuwa vimenakiliwa kama shehena ya samaki, kwenye stakabadhi ya kuzisafirisha.

Changole amesema shehena hiyo ilinaswa mara tu baada ya kuwasili katika mpaka wa Kenya na Uganda, eneo la Malaba.

Msako unaendelea ndani na nje ya mji wa Mombasa, dhidi ya wamiliki wa Pembe hizo za ndovu.

Tangu mapema mwaka huu wawindaji wengi haramu waliokamatwa wameshtakiwa, lakini kuna shinikizo la kutaka adhabu kali dhidi ya wahusika.
XS
SM
MD
LG