Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:28

ElBaradei apinga uchaguzi wa bunge Misri


Mohammed ElBaradei, kiongozi wa upizani Misri
Mohammed ElBaradei, kiongozi wa upizani Misri

Wakristo wa Kanisa la Coptic wapinga tarehe ya uchaguzi wa bunge wakisema itaingiliana na sherehe za Pasaka.

Mmoja wa wapinzani wakuu wa kisiasa Misri ametoa mwito kwa raia kususia uchaguzi ujao wa bunge. Mohammed ElBaradei amesema Jumamosi kuwa anakataa kushiriki katika uchaguzi ulioitishwa na rais Mohammed Morsi mapema wiki hii.

Bwana Morsi ameomba uchaguzi huo uanze Aprili 27, lakini maafisa wametangaza Jumamosi kuwa rais huyo anapanga kubadilisha tarehe hiyo kufuatia upinzani kutoka kwa waumini wa kanisa la Coptic, la Wakristo walio wachache. Tarehe ya Aprili 27 itaingiliana na sherehe za Kikristo za Pasaka.

Lakini Bw. ElBaradei ambaye zamani alikuwa mkuu wa idara ya nuklia ya Umoja wa Mataifa (I.A.E.A.) alisema uchaguzi huo ni kisingizio tu na hutakuwa na matokeo ya hali halisi.

Chama cha Kiislam cha rais Morsi Muslim Brotherhood kimeshinda kila uchaguzi tangu kutimuliwa madarakani kwa rais wa zamani Hosni Mubarak. Lakini mpaka sasa viongozi wengine wa upinzani hawajasema ikiwa wanaunga mkono wito huo wa Bw. ElBaradei au watatii mwito wa rais huyo.
XS
SM
MD
LG