Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:56

Mazungumzo ya amani ya DRC yapiga hatua


Kiongozi wa kundi la waasi wa M23 Askofu Jean Marie Runiga, akizungumza na waandishi habari, Bunagana, Congo, Jan. 3, 2013.
Kiongozi wa kundi la waasi wa M23 Askofu Jean Marie Runiga, akizungumza na waandishi habari, Bunagana, Congo, Jan. 3, 2013.
Mazungumzo ya amani mjini Kampala kati ya serikali ya Jamhuri ya demokrasi ya Congo na waasi wa M23 yamepiga hatua kubwa baada ya pande zote mbili kukubaliana kuhusu kipengele cha kwanza cha ajenda ya mkutano huo ambacho kilikuwa cha kuutekeleza mkataba uliotiwa saini mwaka wa 2009 kati wa serikali ya Congo na waasi wa CNDP.

Na kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda, pande zinazozozana zilikubaliana kuwa mazungumzo yao yatakuwa na maswala manne muhimu yatakayojadiliwa.Kwanza kuutekeleza mkataba kati ya serikali ya Congo na waliokuwa waasi wakati huo wakijiita CNDP ambao baadhi yao waliasi jeshi na kuunda jeshi la M23, pili, usalama nchini Congo, tatu kuzitatua shida za kisiasa, uchumi na jamii na mwisho njia ya kutekeleza makubaliano yatakayofikiwa mjini Kampala.

Kwenye kikao cha kumi na tatu, baada ya kupitia vipengele vyote vya mkataba wa 2009, pande zote mbili zilisema mkataba huo ulikuwa mzuri na kisha kugawa vipengele vya mkataba huo mara tatu. Vile vilivyotekelezwa kamili, vile ambavyo havikutekelezwa kikamilifu na vile ambavyo havikutekelezwa kamwe.

Vipengele 15 vilitekelezwa kikamilifu, 8 vikatekelezwa kiasi, na kumi na mbili havikushughulikiwa hata kidogo.Kutekelezwa kwa mkataba huu kulifaa kufanywa na pande zote mbili lakini kila upande haukutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Kwa mfano, serikali ilitakiwa kuunda kikosi cha polisi wa vijijini kuwalinda raia lakini haikufanya hivyo. Waasi nao walitakiwa kuhakikisha kuwa ikiwa wana shida zozote wanazitatua kulingana na sheria na sio kwa kuchukua silaha lakini walirejelea silaha mwaka uliopita.

Baadhi ya mafanikio ya mkataba huo yalikuwa serikali kuwasamehe waasi wa CNDP na waasi kujiunga na jeshi la serikali ya DRC.
XS
SM
MD
LG