Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 22:10

Morsi afupisha ziara kufuatia ghasia za Cairo


Waandamanaji wanaompinga rais Morsi wakirusha mawe kwa polisi wa kutuliza ghasia mjini Cairo, January 25, 2013.
Waandamanaji wanaompinga rais Morsi wakirusha mawe kwa polisi wa kutuliza ghasia mjini Cairo, January 25, 2013.
Rais wa Misri Mohamed Morsi anafanya ziara fupi kuelekea Ujerumani, jumatano huku matatizo ya kisiasa nchini kwake yakiendelea kwa siku kadhaa za maandamano.

Bwana Mosri alifuta ziara yake ya pili iliyopangwa mjini Paris na kurejea Cairo.
Watu wawili waliuwawa katika mji mkuu jumatano katika mapambano kati ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe na polisi ambao walijibu kwa kutumia gesi ya kutoa machozi. Wataalamu wa huduma za afya walisema waathirika walipigwa risasi lakini haikufahamika wazi nani aliwafyatulia risasi hizo.

Waandamanaji wamekuwa wakiandamana nchini Misri tangu alhamisi siku ambayo ilikuwa ni maadhimisho ya miaka miwili ya ghasia zilizomuondoa madarakani Rais wa zamani Hosni Mubarak. Zaidi ya watu 50 wamekufa tangu maandamano yalipoanza.

Kiongozi wa upinzani Mohamed ElBaradei alitoa wito wa jumatano kuwepo na mjadala wa kitaifa wa kujaribu kusitisha ghasia hizo. Bwana Morsi alikubali jumapili kushiriki katika mazungumzo lakini chama kikuu cha upinzani cha National Salvation Front na makundi mengine yalikataa kushiriki kutokana na hali ilivyo hivi sasa.

Rais alitangaza hali ya dharura ya kitaifa na kutoa amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kuanzia jumatatu jioni ili kujaribu kusitisha maandamano yanayoipinga serikali katika miji ya Port Said, Ismailiya na Suez City.
XS
SM
MD
LG