Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:25

Kerry aidhinishwa kuwa waziri wa mambo ya nje


Seneta John Kerry baada ya kuidhinishwa kuwa mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Januari 29, 2013.
Seneta John Kerry baada ya kuidhinishwa kuwa mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Januari 29, 2013.
Baraza la Senate la Marekani limemwidhinisha Seneta John Kerry kuwa waziri wa mambo ya nje kwa kura 93 dhidi ya 3. Kerry ataondoka kwenye wadhifa wake kama seneta wa jimbo la Massachusetts na kuchukua nafasi ya Hillary Clinton kama mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa serikali ya Rais Barack Obama kwa dunia.

Kuidhinishwa kwa bw. Kerry kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani hakukuwa na shaka. Maseneta wa vyama vyote viwili walimpongeza kabla ya kura hiyo kupigwa Jumanne. Mdemokrat Ben Cardin alielezea wasifu wa Kerry katika kamati ya baraza la senate juu ya maswala ya nje.“Sidhani kuna mtu katika baraza hili aliyehudumu kwa muda mrefu, kusafiri katika maeneo mengi na kukutana na watu akiwakilisha taifa letu katika ngazi ya kimataifa kama yeye.”

Naye seneta Bob Corker wa chama cha Republican alikuwa na maoni sawa na hayo. “Sijui mtu yeyote aliyeishi maisha yake na kujua mengi kuhusu kazi za wizara ya mambo ya nje kama seneta John Kerry.”

Maseneta walikiri kuwa bw. Kerry alijitosa mwenyewe katika maswala ya kimataifa mapema katika maisha yake. Akiwa kijana alipigana katika vita vya Vietnam na baadaye kukemea ukatili alioshuhudia. Kama mbunge, Kerry amesafiri sana katika nchi za nje kwa zaidi ya miongo miwili.

Seneta mdemokrat Robert Menendez ambaye atachukua wadhifa wa Kerry kama mwenyekiti wa kamati ya senate juu ya maswala ya nje, alielezea orodha ndefu ya mafanikio ya bw. Kerry. “Amekuwa mtetezi wa program zinazozuia silaha za nuklia na kibaolojia kufikia mikono ya nchi hatari na magaidi. Alikuwa mtetezi mkuu wa amani kati ya Sudan na Sudan kusini na kutekeleza wajibu muhimu katika kura ya maoni ya mwaka wa 2011. Anafahamika vyema kama mbunge anyefanya kazi na vyama vyote viwili vya kisiasa Marekani.”

Wachambuzi wanasema imani ya Seneta Kerry kuhusu wajibu wa Marekani duniani na matumizi salama ya nguvu zake za kijeshi yanawiana na yale ya rais Barack Obama.
XS
SM
MD
LG