Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 06:14

Uganda imerudisha zaidi ya dola milioni 5 fedha za misaada.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na waandishi.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na waandishi.
Uganda imerudisha zaidi ya dola milioni 5 fedha za misaada zilizoporwa kutoka Ireland kurudi kwa serikali ya nchi hiyo.
Waziri wa mambo ya nje wa Ireland Eamon Gilmore amesema anaamini fedha hizo za fidia zitachangia katika juhudi za serikali ya Uganda kupambana na rushwa. Amesema maafisa wa Ireland kwa sasa watafikiria kuanza tena mpango wao wa misaada uliokuwa umezuiwa kwa serikali ya Uganda.
Zaidi ya dola milioni 5 zilitumiwa vibaya kutoka Ireland mwaka jana na maafisa wa ofisi ya waziri mkuu Patrick Amama Mbabazi ambaye amekataa kuhusika katika hilo.
Wizi huo ulipelekea Uingereza , Denmark na Norway kusimamisha misaada kwa Uganda.
XS
SM
MD
LG