Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:14

Wamisri wapigia katiba kura


Mpiga kura nchini Misri aonyesha alama ya kidole kuthibitisha amepiga kura.
Mpiga kura nchini Misri aonyesha alama ya kidole kuthibitisha amepiga kura.
Nusu ya wapiga kura waliosajiliwa nchini Misri wamepiga kura leo Jumamosi juu ya rasimu yenye utata ya katiba, ambayo imezusha vurugu na maandamano kwa wiki kadha sasa nchini humo.

Wanaume na wanawake walipigia kura zao katika shule tofauti mjini Cairo na mikoa mingine 9.Rais wa Misri Mohammed Morsi pia alipiga kura yake Jumamosi. Wapiga kura wengine watapigia rasimu hiyo kura Jumamosi ijayo Desemba 22.

Kura hiyo imepangiwa kufanyika Jumamosi moja baada ya nyingine kutokana na wito wa kuisusia uliotolewa na wengi katika mfumo wa mahakama nchini humo ambao sharti wasimamie kura hiyo kwa mujibu wa sheria za Misri.

Haijabainika matokeo ya mwisho yatatangazwa lini. Chama cha zamani cha rais Morsi Muslim Brotherhood kinaunga mkono katiba iliyopendekezwa. Morsi alijiuzulu kutoka chama hicho baada ya kuwa rais mapema mwaka huu. Makundi ya upinzani wenye msimamo wa kadri, pamoja na Wakristo wana hofu kuwa katiba inayopendekezwa itahujumu haki zao na kuzipa nguvu zaidi sheria kali za kiislam sharia na haisemi chochote kuhusu haki za wanawake.
XS
SM
MD
LG