Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:58

Kenya na Japan zafanya mkakati wa kupanua bandari ya Mombasa.


baadhi ya wafanyakazi wa bandari ya mombasa wakipakia chakula katika meli
baadhi ya wafanyakazi wa bandari ya mombasa wakipakia chakula katika meli
Upanuzi wa Bandari ya Mombasa unatekelezwa na serikali pamoja na serikali ya Japan, miezi michache baada ya kukamilisha uchimbaji wa kina cha bahari hindi, ili kuwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga katika bandari hiyo.

Mradi huu unahusu ujenzi wa Container Terminal Kilindini, kutokana na shughuli nyingi za upakuaji na usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Mombasa.

Katika uzinduzi huo rais Mwai Kibaki wa Kenya amesema serikali yake imeweka mpango maalum wa kutekeleza upanuzi wa hali ya juu, katika kipindi cha miaka 25.

Rais amesema upanuzi huo pamoja na ujenzi wa bandari ya Lamu, utasaidia wawekezaji kutoka mataifa yote ya kanda hii, ya Afrika Mashariki na Kati.

Ujenzi wa Terminal hiyo mpya utagharimu shillingi za Kenya Billoni 28, na kuongeza nafasi ya kuhifadhi makasha ya mizigo, millioni 1.2.

Awali rais Kibaki akiwa hapa Mombasa aliongoza uzinduzi wa kiwanda cha Kawi –Kipevu, chini ya Kampuni ya KENGN kilichogharimu kwa ujenzi Dola millioni 120.
XS
SM
MD
LG