Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:31

Misri waandamana kupinga maamuzi ya Rais Morsi.


Waandamanaji nchini Misri wakiwa kwenye kambi uwanja wa Tahrir huko Cairo .
Waandamanaji nchini Misri wakiwa kwenye kambi uwanja wa Tahrir huko Cairo .
Rais wa Misri Mohamed Morsi anatarajia kukutana na baraza kuu la sheria wakati majaji wakijaribu kumwomba rais kupunguza madaraka zaidi aliyojipa wiki iliyopita.

Hatua hiyo imepelekea maandamano ya wanaharakati wa upinzani, ambao wameendelea kupiga kambi kwa siku ya nne katika uwanja wa Tahrir wakidai Bw.Morsi abadili uamuzi wake. Wapinzani na waunga mkono wa rais wametaka kuwepo na maandamano makubwa mjini humo Jumanne.

Mwandishi wa VOA Elizabeth Arrott anasema hatua hiyo ya rais inaondoa hatua yoyote ya kuangaliwa juu ya kile anachofanya kama rais.

Amri ya Bw.Morsi inasema uamuzi wake hauwezi kukatiwa rufaa na mahakama na unazuia mamlaka ya sheria ya Misri kulivunja bunge hilo na kamati inayoandika katiba mpya . Wakosoaji wanasema Bw.Morsi anajichukulia mamlaka ya kidikteta kama za mtangulizi wake Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya umma.
XS
SM
MD
LG