Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:10

Museveni na Kagame hawatokubali serikali yeyote kupinduliwa na kundi la waasi


M23 rebels assemble police in Goma
M23 rebels assemble police in Goma
Viongozi wa Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sauti moja wamelitaka kundi la waasi la M23 lililouteka mji wa Goma siku ya Jumatatu usiku, kuondoka nmjini humo na hawatokubali mapinduzi dhidi ya serikali yeyote ya kanda ya maziwa makuu.

Rais Museveni wa Uganda akiuliza watafanya nini ikiwa kundi litakata kuondoka alisema "wataona chamtema kuni".

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:43 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Marais Yoweri Museveni, Paul Kagame na Joseph Kabila walizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo yao na kueleza kwamba ingawa wapiganaji wa M23 wanamadai yaliyo ya haki lakini hawawezi kutumia nguvu kupindua serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Rais Kabila amesema yuko tayari kuyasikiliza malalamiko ya waasi na atafanya kila awezalo kuyashughulikia.

Kwa Upande wake rais Kagame amesema kuhudhuria kwake mazungumzo hayo kunamaanisha anataka amani kwa kanda nzima, bila ya kutilia maanani sula la waandishi habari ikiwa anawaunga mkono wapiganaji wa M23.
XS
SM
MD
LG