Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:54

Kiongozi wa MRC aachiwa kwa dhamana.


MRC demonsrtations in Mombasa
MRC demonsrtations in Mombasa
Kiongozi wa vuguvugu la Mombasa Republican linalopigania mkoa wa Pwani ujitenge kutoka Kenya, Omar Mwamnuadzi pamoja na mke wake na wanae wawili, wameachiwa huru kwa dhamana Jumanne baada ya kuwekwa rumande kwa takriban mwezi mmoja.

Wanachama 37 wa Mombasa Republican walikamatwa na kutupwa gerezani mapema mwezi uliopita wakidaiwa kuhusika na uchochezi katika wilaya ya Kwale kusini mwa Mombasa, ambapo Chifu mmoja aliuawa na walinzi wa mwenyekiti wa MRC Omar Mwamnuadzi.

Miongoni mwa washukiwa hao ni familia ya watu wanne Omar Mwamnuadzi, mke wake Maimuna Mwavyombo, na wanae wawili ambao wamekuwa pamoja gerezani, katika kipindi ambacho nusura mwanae mmoja akose mtihani wake wa kitaifa akiwa gerezani.

Omar Mwamnuadzi aliyejeruhiwa wakati akikamatwa na maafisa wa usalama sasa yuko huru na familia yake kwa dhamana aliyowekewa na mwanasiasa Gideon Mbuvi.

Mbuvi akiwa mmoja wa wabunge chipukizi katika bunge la Kenya, anasema “hatua ya kuwadhamini viongozi wa MRC sio ya kisiasa, bali ni kueneza amani nchini Kenya”.

Jumanne mbunge mwingine kutoka Mombasa Sheikh Mohamed Dor aliyeshtakiwa kwa madai ya uchochezi kuhusu vuguvugu hilo la MRC, lakini akaachiwa kwa dhamana, alikuwa mahakamani Mombasa lakini kesi dhidi yake imeahirishwa hadi Novemba 29.
XS
SM
MD
LG