Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:24

Wakenya watawala mbio za Athens


Mwanariadha Consolater Chemtai Yadaa akikimbia katika mbio za marathon Athens
Mwanariadha Consolater Chemtai Yadaa akikimbia katika mbio za marathon Athens
Wanariadha wa Kenya walitamba tena Jumapili katika mashindano ya mbio ndefu za marathon huko Athens, Ugiriki kwa kushika nafasi sita za kwanza kwa wanaume, wakati mwanadada Cosolater Chemtai yadaa akishika nafasi ya kwanza upande wa wanawake katika muda wa saa mbili, na dakika 40.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja



Raymond Bett akikata utepe Athens
Raymond Bett akikata utepe Athens


Kwa upande wa wanaume Raymond Bett alichukua nafasi ya kwanza katika muda wa 2:11:35 (Bett alishinda mbio hizo miaka miwili iliyopita pia) Paul Kosgei alichukua nafasi ya pili katika 2:12.20 wakati Alex Kirui alishika nafasi ya tatu katika muda wa 2:12.26.

Nafasi nyingine tatu zifuatazo hadi ya sita zilishikwa pia na wakenya Japhet Kipkorir (2:13.31), Peter Biwott (2:14.37) na Charles Ngolepus aliyemaliza katika muda wa saa 2:16.55. Viola Chelangat Kimetto naye wa Kenya alishika nafasi ya tatu kwa upande wa wanawake.
XS
SM
MD
LG