Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:37

Mjadala mkali katiika kikao cha kufunga bunge la 10 Tanzania


Ndani ya bunge la Tanzania mjini Dodoma
Ndani ya bunge la Tanzania mjini Dodoma
Wabunge katika kikao cha mwisho cha Bunge la 10 siku ya Ijuma, walijadili kwa hamasa bila ya kujali itikadi ya vyama walipozungumzia pendekezo binafsi la mbunge Zitto Kabwe wa Kigoma.
Mbunge Kabwe wa chama cha CHADEMA ametaka bunge liunde kamati maalum ili kuchunguza fedha zinazowekwa katika mabeki ya nje na maafisa wa serikali kinyume cha sheria akidaia kuna ushahidi wa kuthibitisha jambo hilo..

Mbunge Peter Msigwa wa Chadema
Mbunge Peter Msigwa wa Chadema


Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa wa chama cha CHADEMA akizungumza na Sauti ya Amerika anasema mjadala ulikuwa wa kusisimua na mkali pale wabbunge walowengi walipinga msimamo wa mwanasheria mkuu wa kutaka kufutilia mbali hoja hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:41 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Anasema baada ya mvutano mkubwa wabunge walikubaliana kwamba inabidi kwa serikali kuwasilisha hoja mbele ya Bunge la 11 ili kulitaka liunde kamati ya kufanya uchunguzi huo kutokana na ushahidi uliyopo kwamba kuna baadhi ya maafisa wa serikali wanahamisha fedha zao kwa njia zisizo halali hadi katika mabenki ya nje hasa Uswisi.
XS
SM
MD
LG