Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:36

Kimbunga Sandy kuleta madhara Marekani


Mike Strobel akijaza mchanga kwenye magunia kwa ajili ya kuweka kwenye eneo lake la biashara.
Mike Strobel akijaza mchanga kwenye magunia kwa ajili ya kuweka kwenye eneo lake la biashara.
Eneo la mashariki mwa Marekani linajiandaa kwa kile watabiri wa hali ya hewa wanabashiri kuwa kimbunga kikubwa kuliko vyote kupata kupiga katika eneo hilo.
Kimbunga Sandy kinaelekea ufukwe wa Atlantic na kinatarajiwa kuungana na vimbunga vingine viwili kutoka kaskazini na kusababisha hali mbaya ya hewa itakayotanda kwa upana wa kilomita 1,200 na kuathiri wakazi milioni 60.

Miji mikubwa imejiandaa kwa kimbunga hicho ikiwemo Washington, Baltimore, New York , Philadelphia na Boston. Ilani zinatolewa kila mahali katike eneo la ufukwe wa mashariki ambapo kimbunga Sandy kinatarajiwa kupiga moja kwa moja kuanzia Jumatatu jioni.
Kimbunga hicho tayari kina upepo wa kilometa 120 kwa saa huku spidi ya juu ikifikia kilometa 165 kutoka kati.

Maafisa wanawaonya wakazi kuhakikisha wanayo maji ya kutosha ya kunywa, vyakula vya makopo na betri na kujiandaa kukaa siku kadhaa bila umeme.
XS
SM
MD
LG