Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 14:42

Siku ya mtoto wa kike yaadhimishwa kimataifa.


Watoto wa kike wa Yemen wakihudhuria shule katika siku yao ya kwanza kuadhimishwa kimataifa..
Watoto wa kike wa Yemen wakihudhuria shule katika siku yao ya kwanza kuadhimishwa kimataifa..
Ripoti mpya inaonesha hali duni ya wasichana wasioelimishwa huku Umoja wa Mataifa ukiadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto wa kike Octoba 11.

Shirika la Plan International linasema huku idadi ya wasichana na wavulana wanaojiunga na shule duniani ikielekea kuwa sawa katika shule za msingi, wasichana wengi hata hivyo hawakamilishi masomo yao.

Shirika la maendeleo ya wasichana linasema wasichana milioni 39 wa kati ya umri wa miaka 11 hadi 15 hawamalizi masomo yao katika shule za msingi.

Mkurugenzi wa shirika la Plan Internatinal Nigel Chapman anasema mara nyingi wasichana wanavyokua familia zao zinawaomba kuchangia kiuchumi na kwa hiyo wengi wanalazimika kuacha masomo yao shuleni.

Anasema tatizo hili ni sugu zaidi barani Afrika. Aidha shirika hilo pia inasema matatizo mengine yanayochangia wasichana kuacha shule ni pamoja na ndoa za mapema na kupata mimba wakiwa bado wadogo.
XS
SM
MD
LG