Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 16:53

Romney abadilisha kauli yake juu ya bima ya afya


Mitt Romney, mgombea kiti cha nafasi ya rais Marekani kupitia chama cha Repuplican
Mitt Romney, mgombea kiti cha nafasi ya rais Marekani kupitia chama cha Repuplican

Asema kama ilivyo kwenye "Obamacare", yeye atahakikisha kuwa wale wenye hali ya magonjwa sugu watakuwa bado na uwezo wa kuhudumiwa kibatibabu

Mgombea nafasi wa kiti cha rais kwa chama cha Repuplican, Mitt Romney amebadili nia sasa na kusema hatobadilisha baadhi ya vipengele vya mpango wa huduma ya afya ulioidhinishwa na Rais Barack Obama, licha ya ahadi zake za hapo awali za kufuta kabisa sheria ya mfumo mzima wa afya ulioidhinishwa na bwana Obama, endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwezi Novemba.

Bwana Romney alisema hayo kwenye kipindi cha “Meet the Press” kinachorushwa na kituo cha televisheni ya ABC nchini Marekani hapo Jumapili akiongeza kuwa sasa anapanga kuutathmini tena mpango huo unaojulikana sana kama “Obamacare” na kuutathmini upya mpango anaopendekeza mwenyewe.

Lakini alielezea kwa kina kuwa kama ilivyo kwenye mpango wa Rais Obama, atahakikisha kuwa wale wenye hali ya magonjwa sugu watakuwa bado na uwezo wa kuhudumiwa kimatibabu na kwamba vijana wataweza kuendelea kubaki kwenye bima ya afya za wazazi wao hadi wafikie umri wa miaka 26.

Alielezea kwamba wakati alipokuwa gavana katika jimbo la Massachusetts, mpango wake wa afya ulikuwa na vipengele hivyo.
XS
SM
MD
LG