Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:46

Obama, Romney waanza kampeni kwenye majimbo muhimu


Rais Obama akiwa kwenye kampeni katika chuo kikuu cha Iowa
Rais Obama akiwa kwenye kampeni katika chuo kikuu cha Iowa

Wagombea wote, Rais Obama na mpinzani wake Romney, wanaitumia siku ya Ijumaa kuwahamasisha wapiga kura katika majimbo ya Iowa na New Hampshire

Rais wa Marekani Barack Obama ameanza siku tatu za kampeni kwenye majimbo yasiyoelekea kwa chama chochote hapo Ijumaa, siku moja baada ya kukubali uteuzi wa ugombea urais kwa chama cha Democrat.

Wagombea wote, Rais Obama na mpinzani wake wa m-Republican, Mitt Romney, wanaitumia siku ya Ijumaa kuwahamasisha wapiga kura katika majimbo ya Iowa na New Hampshire, majimbo mawili muhimu katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Alhamis usiku Bw.Obama aliwaambia wafuasi wake kwenye mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Democrat huko Charlotte, North Carolina kuwa “wanakabiliwa na chaguo la wazi katika kizazi hiki”, pale wanapokwenda kupiga kura mwezi Novemba, “chaguo kati ya njia mbili tofauti kwa wa-marekani”.

Aliwataka wamarekani kujumuika pamoja kuangalia malengo yao katika maeneo ya viwanda, nishati, elimu, usalama wa taifa na punguzo la nakisi akisema yatapelekea “kuongoza upatikanaji wa ajira mpya, nafasi zaidi na kujenga tena uchumi huu kwenye msingi imara”.

Wakati huo huo kampeni ya Romney inatangaza itatoa matangazo mapya 15 ya televisheni Ijumaa yanayolenga juu ya uchumi.

Katika hotuba yake ya Alhamis,Obama alikamilisha kwa kumkosoa vikali mpinzani wake Romney na chama chake cha Repuplican juu ya masuala kadhaa ikiwemo sera za nje, kodi na huduma ya afya.

Alisema kwamba wa-Repuplican wanatoa wito wa kukata kodi kama suluhisho la kila kitu. Lakini alisema yeye haamini kuwapa nafuu ya kodi mamilionea wataleta ajira au kupunguza nakisi ya taifa. Katika suala la sera za nje, alimshutumu Romney kwa kutaka kulirudisha taifa nyuma kuelekea enzi za “majigambo na makosa” katika sera za mambo ya nje.
XS
SM
MD
LG