Alhamisi, Aprili 24, 2014 Local time: 10:57

Katika Picha

ukubwa wa habari - +

Maelfu washiriki mbiyo za Marathon ya Boston

Usalama ulikua mkali kuwahi kutokea, pale watu 35, 755 kutoka mataifa 95 waloshiriki katika mbiyo za marathon za Boston mwaka mmoja baada ya mabomu.

Mafuriko makubwa Dar es Salaam

Wakazi wawili wajaribu kuokoa mali zao kufuatia mafuriko Dar es Salaam

Takriban watu 10 wamefariki na maelfu kupoteza makazi yao kutokana na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua za siku mbili Dar es Salaam

Rwanda yaadhimisha miaka 20 tangu mauwaji ya halaiki

Sherehe za wiki nzima zinafanyika kuwakumbuka walouliwa wakati wa mauwaji ya siku 100 nchini Rwanda mwaka 1994

Wafghanistan wapiga kura kumchagua kiongozi mpya

Wapiga kura wa Afghanistan walijitokeza kwa wingi Jumamosi kuwahi kutokea wakikaidi vitisho vya Taleban na kushiriki katika kumchagua rais mpya atakae chukua nafasi ya Hamid Karzai.

Viongozi wa kidini walaani shambulizi la kanisani Mombasa

Viongozi wa kidini na kisiasa walaani shambulizi katika kanisa la Joy Jesus mtaa wa Likoni , Mombasa ambapo watu wanne waliuwawa na 21 kujeruhiwa

Uchimbaji dhahabu unaongezeka Karamoja Uganda

Baada ya kupoteza mifugo yao, wakazi wa eneo la Karamoja, Uganda wanageukia uchimbaji wa kiwango kidogo cha dhahabu kuweza kumudu maisha yao duni.

Washindi wa tuzo maarufu ya Oscar

Hollywood yatoa heshima kwa wachezaa filamu bora wa mwaka wakati wa tamasha la 86 la kila mwaka la Academy Awards mjini Los Angeles, California.

Waandamanaji wa upinzani wachukua udhibiti wa ikulu Ukraine

Rais wa Ukraine aondolewa madarakani na bunge huku wananchi wachukua udhibiti wa ikulu na afisi zote za serikali.

Mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia

Watu watatu wauliwa na watano kujeruhiwa wakati bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka mbele ya mlango wa uwanja wa ndege wa Mogadishu, Somalia, Alhamisi.

Sherehe za ufunguzi wa michezo ya majira ya baridi ya Olympik Sochi

Sherehe za kusisimuwa kuwahi kufanyika, zilifanyika mjini Sochi, rashia kufungua michezo ya 22 ya Olympik, mbele ya zaidi ya viongozi 40 na kushuhudiwa na mamilioni ya watu duniani.

Polisi wavamia mskiti wa Musa Mombasa

Polisi waliwavamia vijana walokuwa wanakutana ndani ya mskiti wa Musa siku ya Jumatatu na kuwakamata vijana walokuwa ndani.

Mkutano wa viongozi wa AU

Viongozi wa Umoja wa Afrika wakamilisha mkutano wao wa 22 mjini Addis Abeba.

Malalamiko na ghasia za Kiev, Ukraine

Ghasia zimeongezeka katika mzozo wa kisiasa wa miezi miwili nchini Ukraine kati ya wanaounga mkono nchi yao kujiunga na Umoja wa Ulaya na vikosi vya usalama

Filamu na wasani waloteuliwa katika tuzo ya 86 ya Oscar

Filamu na wasani waloteuliwa kuweza kushinda tuzo mashuhuri ya Academy Awards, Oscar, kwa 2014 walitangazwa Alhamisi mjini Los Angeles, California.


Maandamano dhidi ya mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala mashariki ya Congo

Wakazi wa miji ya Mashariki ya Congo wameandamana kulaani mauwaji ya kamanda aliyewamaliza wapiganaji wa M23, na kuanza kuwasaka wapiganaji wa makundi mengine ya waasi.Ghasia za kisiasa Sudan Kusini

Mapigano Sudan Kusini yameenea zaidi ya mji mkuu Juba, ambako yalianza Jumapili katika kile serikali ilichosema ni jaribio la mapinduzi. Mataifa jirani ya IGAD yanafanya juhudi za usuluhishi wa amani.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini azikwa Qunu

Rais wa kwanza muafrika wa Afrika Kusini Nelson Mandela amezika Jumappili katika kijiji cha Qunu jimbo la Cape Mashariki. Maziko yake yanafikisha mwisho siku kumi ya maombolezi ya shujaa wa ukombozi wa nchi yake.